Yanga Yawafanyia Kitu Mbaya Waarabu Kuuboresha Mkataba Wa Mayele


IMEFAHAMIKA kuwa Yanga juzi ilianza mazungumzo na mshambuliaji wake Mkongomani, Fiston Mayele huku ikipanga kuuboresha mkataba wake mpya watakaompa ili abakie kukipiga hapo.


Mayele ni kati ya wachezaji ambao waliopata ofa nono na baadhi ya klabu za nje ya nchi zikiwemo Afrika Kusini na kutoka Uarabuni katika nchi za Saudi Arabia na Iran.


Mshambuliaji huyo tayari yupo nchini tangu juzi Jumanne saa sita mchana akitokea DR Congo alipokwenda katika m
ajukumu ya timu ya taifa iliyocheza mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Gabon ambayo aliifungia timu yake bao.


Mmoja wa Mabosi wa Yanga mwenye ushawishi mkubwa wa usajili, ameliambia Championi Ijumaa kuwa tayari wamempa ofa mshambuliaji huyo ya kuongeza mkataba mwingine wa miaka mitatu ambao unafikia zaidi Sh 500Mil ili abakie hapo.


Bosi huyo alisema kuwa pia uongozi huo umemuwekea ofa ya mshahara inayofikia Dola 12,000 (Sh 28.6Mil) ambao ni zaidi ya ule wa mkataba huo wa mwaka mmoja alionao sasa hivi.


Aliongeza kuwa akipewa ofa hiyo, meneja wake anayemsimamia amekataa mkataba wa miaka miwili na badala yake wasaini mmoja pekee  wenye mshahara wa Dola 15,000 (Sh 35.8Mil).


“Tangu jana (juzi) Jumatano wapo katika mazungumzo na Mayele pamoja na meneja wake anayemsimamia kwa ajili ya mazungumzo ili tufikie muafaka mzuri wa kumbakisha.


“Na tulianza mazungumzo naye mara baada ya yeye kurejea nchini akitokea katika majukumu ya Timu ya Taifa ya DR Congo hiyo ni baada ya yeye kuomba amalize hilo kwanza na baada ya hapo tuanze mazungumzo ambayo tupo katika hatua za mwisho.


“Mazungumzo yanakwenda vizuri na kama mambo yakienda vizuri kwa yeye na meneja wake kukubaliana na ofa yetu, basi atasaini mkataba wa kuendelea kubakia Yanga,” alisema bosi huyo.


Mayele hivi karibuni alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Kabla ya kufanya mazungumzo na klabu yoyote ile, kwanza nitatoa nafasi kwa timu yangu ya Yanga ili kujua ofa yao.


“Mimi ninapenda hela, hivyo nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuanza mazungumzo hayo, mara baada ya kurejea nchini nikitoka kumaliza majukumu yangu ya timu ya taifa,” alisema Mayele.


Naye Meneja wa Habari wa timu hiyo, Ally Kamwe alizungumzia hilo na kusema kuwa: “Tulitegemea kupokea ofa barani Afrika na nje ya Bara la Afrika, ni kweli tumepokea ofa kutoka Klabu nyingi lakini tumeseti mipango yetu.


“Hatupo tayari kupoteza wachezaji wetu bora ikishindikana atazungumza na klabu, hii ni klabu inayotoa fursa ukija ukiagana vizuri na viongozi unapewa baraka unaondoka.”


Mshambuliaji huyo juzi Jumatano mara baada ya kufanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo, katika Ofisi za GSM zilizokuwepo Salamander, Posta Jijini Dar es Salaam alikabidhiwa Tuzo ya Heshima.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1ulwZfF
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story