Azam FC Wafunguka Hali ya Mchezaji wao Aliyevunjika Mkono Kwenye Mechi ya Kujipima



Baada ya kufanya vipimo kwa kina klabu ya Azam Fc imethibitisha kuwa beki wa timu hiyo Edo Manyama ameteguka mkono wake wa kushoto na sio kuvunjika kama ilivyokuwa inaelezwa hapo awali.

Azam Fc kupitia ukurasa wao wa Instagram wameandika...

"Beki wetu @27_edo_manyama aliyepata majeraha kwenye mchezo wetu wa jana Jumatano dhidi ya Stade Tunisien, anaendelea vizuri hivi sasa.

Tofauti na matarajio ya awali tukidhania amevunjika mkono, @27_edo_manyama mara baada ya kupelekwa hospitali na kufanyiwa vipimo kwa kina, imebainika ameteguka mkono wake wa kushoto.

Daktari wa timu yetu, Dk. Mwanandi Mwankemwa, ameweka wazi kuwa, @27_edo_manyama, atakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki moja kabla ya kuruhusiwa kurejea kwenye mazoezi ya kawaida na wenzake".


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/LH18uGx
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI