Kylian Mbappé Apiga Chini Fuko la Hela Kutoka Kwa Waarabu Saudi Arabia


Kylian Mbappé hana nia ya kufungua mazungumzo na Al Hilal kwa sasa. Apiga chini mshahara wa Euro Milioni 700 zaidi ya TZS Trilioni 2 kwa mwaka na zaidi ya TZS Bilioni 36.5 kwa wiki.

Amekataa kufanya mazungumzo na klabu hiyo ya Saudi Arabia baada kutenga kitita cha Euro Milioni 300, dau ambalo halijawahi kutokea kwenye historia ya mpira wa miguu, ili kuinasa saini ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa anayekipiga kunako klabu ya Paris Saint-Germain.

Mbappe mwenye umri wa miaka 24 amewekwa sokoni na mabingwa hao wa Ufaransa baada ya kukataa kusaini mkataba mpya, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kutamatika msimu ujao.

Vyanzo vya karibu na PSG vimeripoti kuwa klabu hiyo imesalia kushawishika kuwa Kylian Mbappé alikubaliana na Real Madrid katika uhamisho wa majira ya joto 2024.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/f74ZEmu
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI