Mke wa Ali Kiba Aibuka na Kulaani Vikali Kauli ya Diamond Kuwa Kashapita nae


Mke wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba, Amina Khalef amelaani kitendo cha Diamond, kumkosea heshima kufuatia kumhusisha kwenye ugomvi wake na mumewe. Na kumfananisha na Mnyama.

Diamond alitumia kauli iliyopokelewa tofauti wakati akimhusisha Amina kwenye majibu ya mfululizo mgogoro wake na Alikiba hali iliyozua sintofahamu na kumuibua Amina na kuandika;

"Ni jambo la kipuuzi, lenye nia mbaya, na la kustaajabisha kabisa kuhusisha watu wasio na hatia katika migogoro/visasi".

"Ninalaani vikali ukosefu wa heshima kwa mwanamke. Bila hisia za heshima, hatuwezi kutofautisha wanaume na wanyama. Ni muhimu kuheshimu haki na hadhi ya kila mtu, bila kujali jinsia au asili yake."

"Utu wema wa kibinadamu hauwezi kukiukwa".


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/8y5DT64
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI