Raya Asimulia Alivyoishi Maisha ya Chini na Barnaba "Sikumlazimisha Abadili Dini"

Raya Asimulia Alivyoishi Maisha ya Chini na Barnaba "Sikumlazimisha Abadili Dini"

Mke wa msanii wa Bongo Fleva Barnaba, Raya amesimulia jinsi walivyoishi kwenye maisha ya hali ya chini kwa takriban miaka minne kabla ya kuingia kwenye ndoa.

Raya ametoa ubuyu huo leo Julai 27, 2023 alipokuwa akifanyiwa mahojiano Wasafi FM ambapo alieleza kuwa, walikutana na Barbaba akiwa ametoka kutendwa na aliyekuwa mpenzi wake.

"Tulishikamana pamoja hakuwa na kitu lakini tuliwkenda mpaka akapata vitu. Tuliishi chumba kimoja kabla ya kuoana, mama alikuwa hapendi lakini nilimsihi amvumilie maana alitoka kuumizwa," alisema.

Raya alisema ilikuwa vigumu mama yake kumuelewa lakini mwisho wa siku kwa kuwa alikuwa ana imani, kweli wakafikia hatua ya kufunga ndoa.

Mke wa Barnaba, Raya ameweka wazi kuwa hakumlazimisha msanii huyo kubadili dini bali yeye mwenyewe ndiye aliamua.

Akizungumza kwenye kipindi cha Mashamsham cha Wasafi FM leo Julai 27, 2023, Raya alisema, Barnaba alipitia kipindi kigumu ambacho yeye ndiye aliyekuwa msaada wake mkubwa kuvuka kwenye kipindi hicho.

Alisema siku aliyokuwa anakwenda kubadili dini, alimfanyia kama sapraiz, hakumjulisha kabla.

"Alikwenda tu na rafiki yangu aliporudi akaniambia nimebadili dini. Nilipokea, tukaingia kwenye ndoa na hakukuwa na pingamizi lolote kutoka kwa wazazi wake licha ya kuwa ni wakristo na Barnaba amenifuata mimi kwenye Uislamu," alisema Raya.




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/3XWf56M
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI