Simba Sc yagoma Katu Katu Kustafisha Jezi ya Jonas Mkude

 

Simba Sc yagoma Katu Katu Kustafisha Jezi ya Jonas Mkude


Klabu ya Simba imeonekana kuendelea kutumia jezi namba 20 ya Jonas Mkude aliyetimkia Yanga ambayo walisema wataistaafisha mpaka atakapopatikana mhitimu mwingine wa timu ya vijana atakayeakisi yale ambayo Mkude almaarufu NUNGUNUNGU amefanya kwa miaka 13 ya utumishi wake klabuni hapo.


Mchezaji mpya wa Wekundu hao wa Msimbazi, Che Fondoh Malone ameonekana akiwa amevalia jezi hiyo wakati klabu hiyo ikiwa kwenye maandalizi ya msimu mpya (pre-season) huko Uturuki.


Awali, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema jezi ya Mkude itastafishwa kwa heshima yake baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 13, lakini baada ya Mkude kijiunga na wapinzani wao yanga, mambo yameonekana kuwa tofauti na ilivyosemwa na Simba hapo awali.


Nini maoni yako kuhusu hili?



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/BGt1ozP
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI