Mpenzi wa Mobetto atua Bongo, Mwamba Afunguka Haya Muhimu

 

Mpenzi wa Mobetto atua Bongo, Mwamba Afunguka Haya Muhimu

 Mpenzi wa Mobetto atua Bongo, Mwamba Afunguka Haya Muhimu

Kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mpenzi wa mwanamitindo Hamisa Mobetto aitwaye Kevin Sowax ametua Dar es Salaam na kupokelewa na mpenzi wake huyo usiku wa kumakia leo.


Kevin amenukuliwa akisema wakati anakutana na Mobetto hakujua kama ni Super Star huku akiweka wazi kumtolea posa mrembo huyo.


Kevin Sowax ambaye ni CEO wa Kampuni ya Twinsk ya nchini Kenya ameshukuru kwa kupata mapokezi makubwa aliyopata kutoka kwa Watanzania.


Sowax amebainisha kuwa amekuja Bongo kwa ajili ya kumsalimia Mobetto na familia yake sambamba na mambo yake ya kibiashara ambayo hakutaka kuyaweka wazi ni aina gani ya biashara.


Aidha, Sowex amesema hakuwahi kukutana na Mobetto tangu mwanzo lakini wamekuwa wakiwasiliana tu kwa njia ya simu lakini sasa wameamua kukutana uso kwa uso.


Mfanyabiashara huyo wakati akihojiwa na vyombo vya habari vya Tanzania, amesema kuwa hana mtoto na anatarajia kupata mtoto kupitia kwa Mobetto.


Kwa upande wake, Mobetto amesema kuwa ameshakuwa mama na mtu mzima hivyo anahitaji kuwa na mwanaume mmoja anayejiheshimu na si kila mwanaume, ili kulinda heshima yake kwa watoto wake.


"Mimi ni mama wa watoto wawili, sidhani kama kila wakati nitakuwa na mwanaume mpya, kama kila kitu kitakwenda sawa basi tutaishi pamoja. Kwa sasa siwezi kusema kwa sababu mambo ya mahusiano ya mambo mengi. Watoto wangu wakikua watakuta hivi vitu mitandaoni," amesema Mobetto.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/O52BHM1
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI