Mudathir Afunguka Ishu ya Simu ya Mkewe Uwanjani

 

Mudathir Afunguka Ishu ya Simu ya Mkewe Uwanjani

Kiungo wa Yanga, Mudathir Yahya amefunguka staili yake ya kushangilia aloitumia baada ya kufunga bao katika mechi ya ufunguzi kwenye Ligi Kuu dhidi ya KMC iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex wakiibuka na ushindi wa 5-0.

Mudathir alionekana akitoa ‘Shin Gurd’ yake mguuni na kuitumia kama ishara ya kupiga simu kuzungumza na mtu.

“Nikiwa sina kitu cha kufanya huwa natumia muda mwingi kuzungumza na mtoto wangu ‘Manha’ pamoja na mke wangu, kabla sijaja kwenye mchezo nilizungumza nao wote na niliwaahidi kufunga ndio maana nilitoa Guard nikafanya kuwa kama simu niwapigie niwaambie nimefunga,” amesema.

Mudathir amekuwa na muendelezo mzuri wa kiwango chake tangu asajiliwe na Yanga kama mchezaji huru baada ya kuachwa na Azam FC.

Kocha Miguel Gamondi amekuwa akionyesha imani kwa kiungo huyo ambaye amekuwa akicheza katika kikosi cha kwanza mara kwa mara chini ya kocha huyo.

Yanga katika mchezo wa ufunguzi kwenye ligi iliibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya KMC huku mabao hayo yakifungwa Dickson Job, Stephane Azizi KI, Hafiz Konkoni, Mudathiri Yahya na Pacome Zouzoua.

Ushindi huo wa Yanga unaingia kwenye rekodi baada ya kufanya hivyo katika mchezo wa ufunguzi katika msimu wa 2013/2014 walipoifunga Ashanti United mabao 5-1



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/fiuZQj3
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI