Mume wa Diva Atoa MPYA 'Siwezi Kuoa Mwanamke Masikini'

 


Mume wa mtangazi maarufu nchini kutoka Wasafi Media, Diva the Bawse aitwaye Abdulrazack amesema kuwa kwa hadhi aliyofikia kwa sasa hawezi kuoa mwanamke masikini ambaye hana pesa.


Abdulrazack ambaye hivi karibuni ilionekana kama ameribuana na Diva amesema mkewe huyo (Diva) ni tajiri hivyo itakuwa jambo la ajabu na aibu kwake kuoa mwanamke ambaye hamfikii pesa Diva.


"Mimi sipendi kulelewa lakini katika Uislamu tumeambiwa unapomuoa mwanamke angalia vitu vinne kwa mwanamke, Uzuri wake, Dini yake, Ukoo wake na mali yake, mimi sitaki mwanamke ambaye hana kitu, hana kazi yoyote kwasababu maisha yamebadilika kuna watoto kwenye ndoa kwahiyo ni muhimu kuwa na Mwanamke ambaye angalau kichwa chake kinafanya kazi.


"Sitaki kuoa mwanamke ambaye ni golikipa kila kitu ananiangalia mimi, kwa levo niliyofikia mimi siwezi kufanya hicho kitu, kwa sasa hivi mshahara ninaowalipa wafanyakazi wangu kwa mwezi haipungui milioni kumi na kuendelea nawezaje kuoa mwanamke ambaye hajishughulishi na chochote? Dunia imebadilika hatuendi hivyo.


"Ni kweli ndugu zangu hawampendi Diva, lakini siwezi kutoa sababu ni mambo ya ndani sana siyo busara kuyaanika lakini yalianza muda mrefu tangu tuko Magomeni. Lakini Diva ni mwanamke mzuri na ni tajiri, watu wengi wanadhani Diva anaishi kwa kutegemea mishahara, wanasahau kwamba jina lake la tatu anaitwa the Boss.


"Maana ya neno (the Boss) ni mtu ambaye anamiliki mali nyingi na siyo hela nyingi tu peke yake, Boss anatakiwa kuwa na ofisi, mali, viwanja na vitu vya thamani mbalimbali ndani yake pia awe na wafanyakazi wengi, huyo ndiyo anaitwa Boss, na hivyo vyote anavyo, na katika mambo yangu manne niliyoangalia kwake ni mwanamke mwenye mali," amesems Abdulrazack.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/V8Wrw73
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI