Rais Samia Akemea Mapenzi ya Jinsi Moja Tanzania



Rais Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Mikoa kuimarisha ulinzi wa vijana dhidi ya kampeni zinazofanywa na baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi ya kueneza mapenzi ya jinsia moja kwa mgongo wa miradi ya maendeleo.

Bila kutaja majina, Rais Samia amesema kumekuwa na mashirika yanapata fedha nyingi lakini lengo kuu ni kuharibu vijana wa taifa.

“Kuna miradi mingi inapata pesa huko chini na ukiangalia mingi inajielekeza kwenye eneo la Afya, Mazingira ili wawapate vijana wetu na kutuharibia. Kuweni na jicho zuri huko chini,” amesema akiwataka viongozi hao kubaini lengo la miradi na kile kinachofanyika katika eneo lao.

“Dunia inabadilika mpaka inasikitisha. Unakwenda kwenye mkutano, analetwa mwanamme kufungua mkutano, anamtambulisha mme wake au anakuja mwanamke anakuja na mke wake … wanatufanyia hivyo ili tuone ni mambo ya kawaida. Nyie wote humu ndani ni waumini haya mambo yanakatazwa,” amesema Rais Samia.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Sd0KTCy
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI