Simba vs Power Dynamos, Yanga vs El Merrikh Ligi ya Mabingwa Afrika

Simba vs Power Dynamos, Yanga vs El Merrikh Ligi ya Mabingwa Afrika



Mabingwa wa Zambia Power Dynamos watachuana na Simba katika mchezo wa raundi ya kwanza ligi ya mabingwa barani Afrika

Ni baada ya Power Dynamos kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya African Stars jana na hivyo kufuzu raundi ya kwanza kwa faida ya bao la ugenini baada ya kuchapwa mabao 2-1 katika mchezo wa mkondo wa kwanza

Mchezo wa kwanza utapigwa Septemba 15 huko Zambia na mchezo wa marudiano kupigwa Septemba 29 jijini Dar es salaam

Simba na Power Dynamos zilichuana kwenye Tamasha la Simba Day, Wekundu wa Msimbazi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Timu hizo zinakutana tena mara mbili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi

Wakati Simba ikichuana na Power Dynamos, Watani zao Yanga wao watachuana na El Merrikh ya Sudan




Jana Yanga ilitinga raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa mabao 7-1 dhidi ya Asas Fc ya Djibout wakati El Merrikh walifuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya Otoho ya Congo Brazaville



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/m7yqpbe
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI