Siri ya Kocha kutimuliwa yafichuka Singida FG



Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Singida Fountain Gate FC, Hans van der Pluijm, amesema kitendo cha kuingiiliwa katika majukumu yake, ndio chanzo cha yeye kuamua kuacha kuendelea kuifundisha timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, imefahamika.

Hata hivyo, uongozi wa klabu hiyo umetoa taarifa ya kuachana na Kocha huyo kutoka nchini Uholanzi, ambaye alipewa mkataba mpya baada yà ule wa awali kumalizika ilipofika Juni 30, mwaka huu.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Hussein Masanza, amesema pande zote mbili zimefikia makubaliano na sasa timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Msaidizi, Mathias Lule.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jijini Dar es salaam zinasema Pluijm amefikia kufanya uamuzi wa kujiuzulu kwa sababu ya kutokubali kuingiliwa majukumu yake ikiwamo upangaji wa kikosi.


Chanzo hicho kiliendelea kusema kitendo cha kukosa uhuru wa kufanya kazi ikiwapo kuingiliwa kupanga kikosi katika mchezo wa marudiano ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika walipocheza dhidi ya JKU.

“Huu nchezo tulipoteza kwa mabao 2-0, ila matokeo ya mechi ya kwanza yalitusaidia kwa sababu tulishinda magoli 3-1, matokeo hayo yametufanya tuendelee kusonga mbele. Sababu ya kujiuzulu ni bosi mmoja wa juu kumwingilia majukumu yake katika kupanga kikosi,” kimeeleza chanzo cha habari hii

Pluijm aliyeiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya nne msimu uliopita na kupata tiketi ya kushiriki michuano hiyo ya CAF na kufanikiwa kufuzu hatua ya kwanza.


Singida Fountain Gate imekuwa timu ya kwanza kuachana na kocha wake tangu kuanza kwa msimu wa Ligi Kuu Bara hapo Agosti 15, mwaka huu.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/WP3KHLV
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI