Mashabiki Power Dynamos Watua Dar Kwa Kishindo Kuhakikisha SIMBA Anashikwa Mkia

Mashabiki Power Dynamos Watua Dar Kwa Kishindo Kuhakikisha SIMBA Anashikwa Mkia


Mashabiki wa Klabu Bingwa nchini Zambia Power Dynamos wapo safarini kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuishangilia timu yao, itakayokabiliwa na mchezo wa Mkondo wa pili wa kuwania kufuzu Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, dhidi ya Simba SC.

Miamba hiyo itakutana Jumapili (Oktoba Mosi) katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam, huku ikikumbuka matokeo ya sare ya 2-2 yaliyopatikana kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza uliopigwa Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia Jumamosi (Septemba 16).

Klabu ya Power Dynamos imethibitisha kusafiri kwa Mashabiki hao kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, kwa kuweka picha inayowaonesha wakiwa safarini kwa njia ya barabara.

Hatua hiyo ni kama majibu kwa Mashabiki wa Simba SC ambao walisafiri kuelekea Ndola, Zambia kwa lengo la kuishangilia timu yao ikicheza ugenini na kuambulia matokeo ya sare ya 2-2.

Wakati Mashabiki wakiendelea na safari, Kikosi cha Power Dynamos kinatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam leo Alhamis (Septemba 28) kwa ndege ya shirika la ndege la Tanzania ‘ATCL’



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/W7UXRQY
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI