TANZIA: Mtoto wa Mandela afariki dunia…




Mjukuu wa shujaa wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Nelson Mandela, Zoleka Mandela, amefariki dunia baada ya kuuguwa saratani akiwa na umri wa miaka 43, familia yake imethibitisha.

Anafahamika kwa kuelezea mapambano yake ya muda mrefu dhidi ya ugonjwa huo wa saratani.

Alilazwa hospitalini Jumatatu kama sehemu ya matibabu yake na amefariki akiwa amezungukwa na marafiki na familia, kwa mujibu wa Zwelabo Mandela.


Alikuwa mtoto wa binti mdogo wa Mandela, Zindzi Mandela, na mume wake wa kwanza, Zwelibanzi Hlongwane.

Familia hiyo ilisema uchunguzi wa hivi majuzi kuhusu saratani, ulionyesha ilivyokuwa imeathiri nyonga, ini, mapafu, ubongo na uti wa mgongo.

“Tunaomboleza kumpoteza mjukuu mpendwa wa Mama Winnie na Madiba,” Wakfu wa Nelson Mandela uliandika kwenye mitandao ya kijamii.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/M59FrHq
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI