TARURA waonywa uchimbaji mashimo barabarani

TARURA waonywa uchimbaji mashimo barabarani


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewataka watendaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini – TARURA, kuacha utaratibu wa kuchimba barabara na kuziacha na mashimo kwa muda mrefu bila kuyafukia.

Aidha, pia ameonya kuwa atawaondoa katika nafasi zao watendaji wa TARURA pamoja na Mameneja wa TARURA wa Mikoa na Wilaya pale ambapo mashimo hayo yataachwa wazi hadi wiki mbili bila kuyafukia kwa utaratibu unaofaa.

Hata hivyo, Waziri Mchengerwa amesema yapo mashimo yamechimbwa na kuachwa wazi kwa mwezi mzima, hali inayosababisha adha kwa watumiaji wa barabara na wakati mwingine kusababisha ajali.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/OJN6y0v
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

Zifahamu staili 6 za Kufanya Mapenz

JINSI YA KUMVUTIA MVULANA/MSICHANA HADI KUWA MPENZI WAKO

Nikiwa na Msichana Namkinai, Hivi Nina Pepo au ni Tamaa tu?