Viingilio Simba vs Power Dynamos Ligi ya Mabingwa

Viingilio Simba vs Power Dynamos Ligi ya Mabingwa


Klabu ya Simba leo imetangaza viingilio vya mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutnga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mchezo dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa uwanja wa Azam Complex, Jumapili Oktoba 1 2023

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema maandalizi ya mchezo huo yanaendelea vizuri ambapo ni wachezaji watatu tu ambao watakosekana kutokana na changamoto za majeruhi

"Mchezo dhidi ya Power Dynamos utachezwa siku ya Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex. Tumeamua kucheza saa 10 sababu michezo mingi hapa karibuni tumecheza muda huo hivyo hatukutaka kubadili muda lakini pia Jumatatu itakuwa siku ya kazi hivyo tunataka watu wawahi kurudi nyumbani"

"Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui"

"Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo," alisema Ahmed

Aidha pamoja na kutangaza viingilio vya mchezo huo, Ahmed amewataka mashabiki kununua tiketi zao mapema ikizingatiwa uwanja wa Azam Complex unachukua takribani mashabiki elfu saba tu

"Viingilio tumeweka rafiki lakini pia tukubaliane uwanja wa Azam Complex ni uwanja mdogo. Kwenye mchezo kama huu msimu uliopita tuliingiza watu 47,000 lakini sasa tutakuwa na mashabiki 7,000. Mashabiki wanaotaka kuwepo uwanjani wanunue tiketi haraka"

"Tiketi za Mzunguko ni Tsh. 10,000, VIP B ni Tsh. 30,000 na Platinum ni Tsh. 150,000 ambayo utapata zawadi, usafiri, chakula ukiwa uwanjani. Watu wanasema Chamazi ni mbali lakini watu wa Platinum Chamazi sio mbali maana wana basi na escort"

"Power Dynamos wanatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi majira ya saa 12 jioni na shirika la ndege la ATCL. Waamuzi wanatarajia kufika Tanzania tarehe 30 Septemba,"  alisema Ahmed



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/OPQtTkp
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI