Azam FC Pamoja na Fei Toto Wao Wapokea Kichapo Cha Nguvu Kutoka Kwa Namungo

 

Azam FC Pamoja na Fei Toto Wao Wapokea Kichapo Cha Nguvu Kutoka Kwa Namungo

Azam FC Pamoja na Fei Toto Wao Wapokea Kichapo Cha Nguvu Kutoka Kwa Namungo

Namungo FC kwa mara ya kwanza jana Oktoba 27, 2023 walipata ushindi wa kwanza dhidi ya Azam FC kwa kuitandika 3-1.

Namungo walianza kupata goli la kwanza dakika za mapema kabisa za mchezo kupitia kwa Buswita dakika ya 10 na dakika ya 19 wakaweka chuma ya pili kupitia kwa Manyanya kisha dakika ya 50 wakaweka mchi wa tatu kupitia kwa Lusajo.

Bao la kufutia machozi la Azam lilifungwa na Ayubu Lyanga dakika ya 70 ya mchezo.

Namungo wametoka mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu hadi kushika nafasi ya 12 wakifikisha alama 6 baada ya kucheza michezo saba. Wamepata sare michezo mitatu, wamefungwa mitatu na kushinda mmoja.

Kwa upande wao Azam, wapo nafasi ya 3 wakiwa na alama zao 13. Kinara wa msimamo ni Yanga SC mwenye alama 18 akifuatiwa na Simba mwenye alama 15 akiwa na gepu la michezo miwili kwa Yanga. Simba amechezo michezo mitano, Yanga saba.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Kpf7yqO
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI