Baba Amnyonga Mwanaye Kwa Kamba Ya Viatu Na Kupiga Naye Selfie – Aacha Ujumbe Mzito

 
Mkazi wa Mtaa wa Kota, Kata ya Mlandege Mkoani Iringa, Goodluck Mgovano aliyekadiriwa kuwa na umri wa miaka 33 anadaiwa kumuua Mtoto wake Alvini Mgovano mwenye umri wa miaka minne kwa kumnyonga na kamba ya viatu huku akijirekodi kwa simu yake ya mkononi wakati akimnyonga Mtoto na alipomaliza akapiga selfie na mwili wa Mtoto na kuacha ujumbe ulioelekeza wapi Mtoto huyo azikiwe.

Kwa mujibu wa taarifa za Majirani Goodluck alijifungia ndani na Mtoto wake na kumnyonga nyuma ya mlango kwa kutumia kamba ya viatu huku akirekodi tukio hilo kwa simu yake ya mkononi na baada ya hapo alimlaza kitandani na kupiga nae tena picha (Selfie) na kutokomea kusikojulikana na bado anatafutwa “Simu yake yenye picha na video aliiacha hapohapo nyumbani na kwa sasa ipo mikononi mwa Polisi”

Mtuhumiwa aliacha ujumbe uliosema “Chanzo cha mauaji haya ni ugomvi uliotokea kati yangu Mimi na Mke wangu mnamo Oktoba 6, 2023 na mimi naenda kujiua na nataka mimi na Mwanangu tuzikwe Kijiji cha Itendulinyi”

Diwani wa Kata ya Mlandege, Jackson Chaula amesema Mtuhumiwa alikuwa anafanya kazi ya ubebaji mizigo katika magari lakini hakuwa na shida yeyote, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa Alfred Mwakalebela amekiri kupokea mwili huo na kusema mwili huo ulikuwa na makovu ya shingoni.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Mo6sAE9
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI