Billnass kumlipia faini Ally Kamwe TFF

 


Msanii wa muziki Bongo Fleva ambaye pia ni mfanyabiashara na shabiki kindakindaki wa Klabu ya Yanga, William Lyimo maarufu kama Billnass amesema atalipa faini ambayo Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ally Kamwe amepigwa na Bodi ya Ligi.

Kamwe amepigwa faini ya Tsh million moja na Kamati ya Bodi ya Ligi kwa madai ya kumdhalilisha mwamuzi, Tatu Maologo mtandaoni.

Kupitia mtandao wa Instagram baada ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Singida FG FC na Simba Sc ambapo Simba ilishinda kwa bao 2-1, Kamwe alipost picha ya mwamuzi Tatu Malogo kisha akaiwekea wimbo wa Billnass uitwao 'Maokoto' jambo lililotafsriwa kuwa mwamuzi huyo kuhusishwa na kupokea rushwa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Billnass ameandika; "Pole sana (Ally Kamwe). Ila sisi kama Nenga Tronics kwa kidogo tulichojaaliwa tunaomba tumalize sisi (faini) japo tunajua (faini) iko ndani ya uwezo wako. Lakini najua MAOKOTO ni wimbo wako pendwa," amesema Billnass.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/E5TMAmg
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI