Chanzo cha Ajali ya Basi na Lori iliyouwa Watu 18 Mkoani Tabora



Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amesema chanzo cha ajali ya Basi kugongana na Lori na kupelekea vifo vya watu 18 ni uzembe wa Dereva wa lori kujaribu kulipita gari jingine bila kuchukua tahadhari.

Amesema, basi la kampuni ya Alfa lilikuwa likitokea Mwanza kuelekea Dar es Salaam na liligongana uso kwa uso na Lori la mafuta la kampuni ya GBP katika Kijiji cha Undomo Wilayani Nzega Mkoani Tabora.


Kamanda Abwao amesema waliofariki ni wanaume 13, wanawake 5 na wengine 36 wamejeruhiwa, idadi ambayo inajumuisha watoto wadogo ambao miili yao imehifadhiwa na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Nzega.

Awali, Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu – LATRA, Nelson Mmari alisema abiria waliopanda basi hilo ni 49, huku Serikali ikifanya jitihada za matibabu kwa majeruhi.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/GExyLoz
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story