Kiungo mshambuliaji wa Yanga STEPHANIE AZIZI KI ameigomea timu hiyo Kuongeza mkataba


Kiungo mshambuliaji wa Yanga STEPHANIE AZIZI KI ameigomea timu hiyo Kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo ya pale Jangwani ikumbukwe Mchezaji huyo alisajiliwa na Yanga tarehe 24/08/2022 akitokea Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast ambapo alimaliza msimu akiwa na timu hiyo kama mchezaji bora wa msimu wa ligi kuu nchini humo mara baada ya kutua yanga alisaini kandarasi ya miaka 2 kuitumikia timu hiyo kwa mshahara wa milioni 27 kwa mwezi na ada ya uhamisho wa dola laki mbili na nusu.

Baada ya kuwa na msimu mzuri kwa kumaliza na mabao 10 na assist 7 msimu uliopita kisha kuanza vyema msimu huu mpaka sasa ana goli 6 na assist 7 uongozi wa Yanga ulianza mazungumzo tangu Jana ya kumboreshea maslahi na kutaka kumuongezea mkataba tena wa miaka miwili ili asalie jangwani hapo hadi 2026 mchezaji huyo amegoma kuhusu jambo hilo la kuongeza mkataba jambo ambalo limewafanya viongozi wa Yanga kukuna kichwa na kuwapa wasi wasi na hofu kubwa na kisha kujiuliza je anataka kwenda timu gani mchezaji huyo kama ikisalia hivyo inamaana Ataondoka Yanga mwakani akiwa kama mchezaji huru na yanga haitopata faida yoyote ile.

MZEE WA #ZACUBA DOCTOR MOHAMEDI HAMISI Nimepenyezewa habari za uhakika na chanzo cha karibu sanaa cha mchezaji huyo kikisema kuwa mchezaji huyo atabaki kucheza Tanzania 🇹🇿 msimu ujao lakini sio kwenye timu ya Yanga swali je unahisi Azizi ki atatimkia wapi kama hataki kubakia Yanga ila atabakia Tanzania 🇹🇿 akitumikia klabu nyingine?


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/XZn7w3Y
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI