Kocha Gamondi Afunguka Haya Kuhusu Mchezo wa Yanga na Singida Fountain Gate

Kocha Gamondi Afunguka Haya Kuhusu Mchezo wa Yanga na Singida Fountain Gate

 


Kocha Mkuu wa Kikosi cha Yanga, Miguel Gamondi, amezungumzia mipango yake kuelekea mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Ijumaa ya Oktoba 27, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 12:30 jioni.

Akizungumzia mchezo huo, Gamondi amesema, wachezaji walitumia nguvu kubwa katika mchezo uliopita tulioshinda magoli 3-2 dhidi ya Azam, hivyo anatumia siku tatu za maandalizi kuwaweka sawa wachezaji ili kuendelea na malengo ya kukusanya alama tatu.

“Tumetoka kucheza mechi ngumu sana dhidi ya Azam, wachezaji walitumia nguvu kubwa, tunajaribu kuwa na mazoezi mazuri ndani ya siku tatu hizi kuona utimamu wao umefikia wapi.

“Siwezi kusema kama kutakuwa na mabadiliko ya kikosi, hilo litategemea sana tutakachokiona mazoezini. Mechi ya Singida ni ngumu na tunahitaji kuingia kamili ili kuweza kupata pointi tatu,” alisema Gamondi.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/kRuXPSw
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI