Miji miwili ya Misri yashambuliwa kwa makombora
Makombora yamepiga miji ya Taba na Nuweiba iliyoko Bahari ya Sham nchini Misri siku ya Ijumaa, vyanzo na maafisa walisema, na kujeruhi watu sita na kuonyesha hatari ya kuenea kwa mzozo wa kikanda unaotokana na mzozo wa Israel na Gaza.
Jeshi la Israeli limelilaumu "tishio la anga" katika eneo la Bahari ya Sham: ikielezea uwezekano huo kufanywa na wanaharakati wa kundi la Wahouthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran ambalo linajulikana kwa kutumia ndege zisizo na rubani.
Msemaji wa jeshi la Misri Kanali Gharib Abdel-Hafez alisema "Drone isiyojulikana" ilianguka kwenye jengo lililo karibu na hospitali na kuwajeruhi watu sita katika mji wa Taba ulio kwenye mpaka na Israel, majira ya asubuhi.
Baadaye, kombora jingine lilidondoka karibu na kiwanda cha umeme kilichopo katika eneo la jangwani katika mji wa Nuweiba ulioko takriban kilomita 70 kutoka mpakani, vyanzo viwili vya usalama vya Misri vililiambia shirika la habari la Reuters, na kuongeza kuwa bado wanakusanya taarifa zaidi.
Hakukuwa aliyedai kuhusika.
Miji ya Taba na Nuweiba, yote ipo katika Peninsula ya Sinai nchini Misri, na ni maarufu kwa watalii.
Mashahidi katika maeneo yote mawili, ambao hawakutaka majina yao kutajwa, walithibitisha kusikia milipuko na kuuona moshi ukitanda huku ndege za kivita za Misri zikiruka juu.
Picha zinazosambaa mtandaoni na katika vyombo vya habari vya Misri zilionyesha jengo lililoharibiwa na magari yaliyolipuliwa.
Misri imekuwa na nafasi muhimu ya upatanishi katika mzozo huo uliozuka wakati Hamas ilipoishambulia Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua zaidi ya watu 1,400, wengi wao wakiwa raia, na kuwachukua mateka zaidi ya watu 220, kwa mujibu wa takwimu rasmi za Israel.
Mashambulizi ya Israel huko Ukanda wa Gaza tangu wakati huo yameua zaidi ya watu 7,000, pia wengi wao wakiwa raia, kwa mujibu wa wizara ya afya katika eneo la Palestina linaloongozwa na Hamas.
Jeshi la Israel limekuwa likitumia ndege zisizo na rubani kulifuatilia eneo la Gaza wakati Hamas na makundi mengine yenye silaha, ambayo yamekuwa yakirusha makombora kuelekea Israel, yamekuwa yakituma ndege zao.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/sdlVyMR
via IFTTT
Comments
Post a Comment