Serikali Yafunguka Tetesi za Uwepo wa Kiwanda Cha Mayai Goba Dar es Salaam

 


Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imekanusha taarifa za uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mayai katika eneo la Goba wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam kama ilivyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii 



Hatua hiyo imekuja baada ya uwepo wa picha zinazosambaa mitandaoni iliyoambatana na maneno yasemayo, "Serikali hailali kama alivyo shetani halali!! wanajua kabisa kwa sababu shetani halali kwahiyo kuna mambo mabaya atayatenda tu!! kiwanda cha mayai Goba kwa wachina kimekamatwa sasa hayo mayai yote sijui yametagwa na kuku gani? tusubiri yanayojiri, usikie teknolojia ilivyo hapo ndiyo utakapojua kwanini kila mtu ana kitambi,".


Aidha Wizara imesema kwamba inawatoa hofu wananchi kuwa imefuatilia suala hilo kwa kina na kujiridhisha kuwa tarifa hizo sio za kweli, ni upotoshaji na hivyo kuitaka jamii kuipuuza.


Wizara pia imesema taarifa hizo zimetengenezwa kwa nia ovu ya kuharibu tasnia ya kuku nchini inayokuwa kwa kasi na kwamba katika kufuatilia zaidi, Wizara imebaini kuwa picha hiyo ya mayai mengi iliyotumiwa ilionekana kwenye mitandao ya kijamii mwaka 2016 na haikupigwa hapa nchini.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/PZUljDG
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story