TCRA Haijakataza Matumizi ya VPN



Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia kwa Mkuu wake wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Rolf Kibaja imesema taarifa kwa Umma iliyotolewa juzi October 13,2023 haijakataza matumizi ya VPN kama baadhi ya Watu wanayopotosha kupitia mitandao ya kijamii.

Kibaja amesema kwamba TCRA imetoa utaratibu kwa Watumiaji wa VPN kutoa taarifa za matumizi ya VPN lakini haijazuia matumizi ya VPN “Watu wanaoshiriki kutoa taarifa kuhusu VPN wataendelea na shughuli zao kama kawaida kupitia VPN”

Kibaja amesema "Ni muhimu kwa Watumiaji wa VPN kutoa taarifa kwakuwa kusajili huduma ya VPN ni kama kujisajili kwa namba ya simu, Nchi nyingi zilizoendelea duniani zimechukua hatua kama hizi kuimarisha usalama mtandaoni, kama vile Uturuki, India, Belarus, Misri, China, na nchi nyingine”

“Ni muhimu kufahamu kuwa matumizi ya VPN nchini hayakatazwi bali yanapewa utaratibu rasmi, kutoa taarifa hizo hakuna gharama yoyote ya malipo na hakuingilli masuala ya faragha wala usalama wa watumiaji husika., TCRA inaendelea kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kuhakikisha usalama katika mtandao sambamba na Watumiaji wa mtandao kuendelea kuwa salama”


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Fs8el32
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI