TMA yasisitiza uwepo wa El Nino, yatabiri mvua kubwa mikoa 15TMA yasisitiza uwepo wa El Nino, yatabiri mvua kubwa mikoa 15




MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imesisitiza uwepo wa mvua za El Nino na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kukabiliana na athari zinazoweza kutokea.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chan'ga.
Aidha TMA leo  imetoa utabiri wa uwepo wa mvua za wastani mpaka juu ya wastani kwa mikoa inayopata mvua mara moja kwa mwaka ambayo ni Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara, Ruvuma na  eneo la  Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

Akizungumza wakati akitoa utabiri huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladislaus Chan'ga amesema katika kipindi cha nusu ya msimu (Novemba 2023 hadi Januari, 2024) kinatarajiwa kuwa na mvua nyingi ukilinganisha na nusu ya pili (Februari hadi Aprili 2024), uwepo wa El-Niño unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika mvua za msimu.

Dk. Chang’a amebainisha athari zinazoweza kujitokeza ikiwa ni vipindi vya unyevu wa kuzidi kiasi pamoja na mafuriko vinaweza kujitokeza na kuathiri ukuaji wa mazao na miundombinu ya kilimo, vile vile, kina cha maji katika mito na mabwawa kinatarajiwa kuongezeka.

Amesema katika mikoa hiyo inayopata mvua mara moja kwa mwaka, mvua zinatarajiwa kuanza kunyesha wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba na wiki ya kwanza ya mwezi Novemba na zinatarajiwa kumalizika wiki ya nne ya mwezi Aprili mwaka 2024.


Katika hatua nyingine, Dk. Chang’a amefafanua kuwa Msimu wa Vuli kwa miezi ya Oktoba hadi Disemba, 2023 katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dar es Salaam, kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba) utabiri wake ulitolewa agosti 24 mwaka huu mvua hizo zimeshaanza katika maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria, Pwani ya kaskazini na baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki kama ilivyotabiriwa.

Aidha, ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya Novemba na Disemba, 2023. vilevile, mvua za nje ya msimu zinatarajiwa katika mwezi Januari na Februari, 2024.

"Watu wandelee kuchukua tahadhari kama tunavyosisitiza , mifumo ya hali ya hewa pia bado inaonyesha uwepo wa El Nino, wananchi na Mamlaka husika ziendelee kuchukua tahadhari," amesema Dk Chang'a.


Amesema moja ya athari wanazozitarajia ni uwepo wa mafuriko katika mikoa mingi hivyo tahadhari zichukuliwe kukabiliana na athari zake.

Mara ya mwisho mvua za El Nino zilinyesha msimu wa mwaka 2018/2019 ambayo hata hivyo ilikuwa El Nino dhaifu kulinganisha na El Nino ya mwaka 1997-1998


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/lh4rKTJ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI