Al Ahly yakeshea video za Yanga, waingia ubaridi




AL Ahly watatua kwenye ardhi ya Tanzania leo kuikabili Yanga Jumamosi jioni. Lakini kiungo wao,Allou Dieng amekiri kwamba wako kwenye presha kubwa kuelekea mchezo huo.

Amekiri kwamba wamepata fursa ya kuipekua Yanga haswa kwenye mechi ya mwisho dhidi ya CR Belouizdad lakini wamegundua ina mabadiliko makubwa kiuchezaji, lakini kinachowaumiza ni kukosa matokeo kila wanapokanyaga Kwa Mkapa.

Dieng ambaye ni panga pangua, alisema bado wanajitafuta kwa jinsi gani watapata matokeo ya ushindi kwenye ardhi ya Tanzania kwasasa kwani tangu ametua Ahly hajashinda Kwa Mkapa na mara ya mwisho walisare katika mechi ambayo waliamini watashinda.

“Tulipokuja Tanzania mara ya mwisho kucheza na Simba tuliona kwamba ni mchezo ambayo tulistahili kushinda kwa jinsi tulivyoianza mechi lakini baadaye tukafanya makosa ya kuruhusu mabao mawili ya haraka,” alisema Dieng.

“Tunakuja tukijua kwamba tunakwenda kucheza uwanja mgumu kwasasa kwetu tunataka kuhakikisha kwamba tunabadilisha haya matokeo ingawa tunajua tunakwenda kukutana na timu nyingine ngumu,”alisema Dieng na kukiri kuwa Yanga ina wachezaji bora ambapo amekuwa akipata taarifa nyingi za ubora wao kwa kumfuatilia kipa wa timu hiyo Djigui Diarra ambaye ni rafiki yake.

“Nimekuwa nikiifuatilia Yanga kupitia Djigui (Diarra) kuna taarifa nyingi nzuri kuhusu wao, ndani yake nimekuwa naona wana timu bora wanafanya vizuri na wachezaji wengi ni wazuri hii inaifanya mechi yetu na wao kuwa ngumu.

“Ukiangalia Diarra ni kipa mzuri na mkubwa wapo wachezaji wengine lakini kubwa ni hii kucheza fainali ya shirikisho msimu uliopita kwahiyo tunawaheshimu lakini tutapambana nao kutafuta alama tatu.” 


Ahly mara ya mwisho kuja nchini ilikuwa ni Oktoba 20 walipocheza dhidi ya Simba mchezo ambao licha ya Waarabu hao kuanza kwa kasi kwa kutangulia kupata bao lakini wekundu hao walisawazisha kisha kupata bao la pili na mchezo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Ahly wamewahi kupoteza mara moja mbele ya Yanga kwenye mechi zao 10 ilikuwa Machi mosi 2014 kwa bao 1-1 ambapo baadaye walikutana tena Aprili 9,2016 na kutoka sare ya bao 1-1.

Waarabu hao pia wakapoteza mara mbili dhidi ya Simba kwa miaka miwili tofauti matokeo kabla ya kupata sare msimu huu.

KOCHA AINGIA UBARIDI

Kocha wao Mkuu, Marcel Koller ameliambia Mwanaspoti kuwa;

“Tutajaribu kuonyesha kilichokuwa bora kwa ajili ya kupata matokeo mazuri, Yanga ni timu yenye wachezaji wazuri wenye uwezo mkubwa kwa sababu tulipata nafasi ya kuifuatilia mechi yao na Belouizdad hivyo ni lazima tujipange sana.”

Kwa upande wa Ofisa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Gamal Gabr alisema timu hiyo itatua nchini leo na wachezaji 25 huku nyota watatu, Taher Mohamed, Antony Modeste na Mahmoud Metwaly wakiwa kwenye hatihati ya kuukosa mchezo huo muhimu.

Timu hizo zilizopo Kundi D zinakutana katika mchezo huo utakaopigwa saa 1:00 usiku huku Al Ahly ikitoka suluhu katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Smouha na kufikisha pointi 14 nyuma ya vinara Pyramids yenye pointi 16. Yanga inahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kundi hilo kwani baada ya hapo itakwenda Ghana.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/SyKVwk5
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI