Haji Manara "Barbara Alivyoteuliwa tu Kuwa CEO wa Simba Nilimpigia Mo Dewji Nataka Kuacha Kazi"



Simba walikuwa wananilipa mshahara usiokuwa na mkataba maalumu ,Yanga wamemiwekea mzigo mezani ,mapenzi ya mashabiki wa Yanga ni makubwa kuliko yale ya Simba sasa kwanini hiyo timu mimi nisiipende “

“Barbara wakati anateuliwa kuwa mjumbe wa bodi ,wakati huo CEO wetu alikuwa Senzo na Senzo alikosa raha kwa sababu ya kuingiliwa majukumu yake ,baadae Senzo akaenda Yanga Barbara akawa CEO na mimi nilishaona huyu hatuwezi kufanya kazi pamoja “

“Alivyoteuliwa tu nikampigia simu Dewji kumueleza kwamba nataka kuacha kazi ,siwezi kufanya kazi na Barbara tutagombana ,wakatuitishia vikao zaidi ya saba, kuna siku uongozi ukasema umeshindwa na wote wanatuhitaji kakaeni wenyewe “

“Nilikaa kikao na Barbara toka saa 10 jioni mpaka saa 7 usiku ,shida kubwa Barbara aliingia pale na kutaka kuonyesha power yangu ni ndogo”


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/RpkO9tj
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI