Yanga Yafungwa 3 Bila na CR Belouizda Klabu Bingwa Afrika

 

Yanga Yafungwa 3 Bila na CR Belouizda Klabu Bingwa Afrika

Wananchi Yanga SC ni kama wamekaribishwa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuchezea kichapo cha goli 3-0 kutoka kwa CR Belouizdad.


Yanga wameingia hatua ya Makundi Klabu Bingwa Afrika msimu huu baada ya kupita miaka mingi kadhaa bila kucheza michuano hiyo mikubwa zaidi kwa levo ya klabu.

SOMA PIA: 

Yanga wakiwa ugenini nchini Algeria, walikubali kuchezea kichapo hicho ukiwa ni mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi.


Magoli ya Belouizdad yamewekwa kimiani na Benguit dakika ya 10 ya mchezo na Abdul dakika ya 45. Chuma ya tatu ilimaliziwa na Jalou dakika ya 90 ya mchezo.


Magoli hayo mawili yalitosha kuwaangamiza Yanga na hadi filimbi ya mwisho inapulizwa, Belouizdad 3-0 Yanga.


Kwenye kundi lao, CR wanaongoza wakiwa na alama 3 huku ukisubiriwa mchezo kati ya Al Ahly na Medeama utakaopigwa kesho ili kutoa picha ya kundi lao baada ya mechi zao za kwanza.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/sxhKCJN
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI