Ajali ya Basi iliyouwa 13: Ndugu waitwa kutambua miili
Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki imesema Mamlaka za Jamhuri ya Zambia zilitoa taarifa kuhusu ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria aina ya Volvo la Kampuni ya Mukombe Luxury lenye namba za usajili DK72 HH GP linalofanya safari kati ya Afrika Kusini na Tanzania, lililogongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T850 DSN la nchini Tanzania.
Katika ajali hiyo iliyotokea katika Wilaya ya Serenje, Jimbo la Kati nchini Zambia Desemba 26, 2023 ilisababisha vifo vya watu 13 na majeruhi 42 wa mataifa mbalimbali, ikiwemo Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Afrika Kusini, Botswana na Zambia.
Watanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Oscar Mwamulima (37), mwenyeji wa Mbozi, Mbeya, Said Mohamed Dige (20), mwenye hati ya Kusafiria Na. TAE403048, mzaliwa wa llemela, Mwanza.
Wenngine ni Peter Blass Munishi (48), mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE378465, mzaliwa wa Siha, Kilimanjaro na Bashiru Salum Kiluwa (42) aliyekuwa dereva msaidizi wa Basi mwenye Hati ya Kusafiria Na. TAE173695, mzaliwa wa Lushoto, Tanga.
Taarifa hiyo imeendelea kuwataja Rashid Athumani Salehe, Dereva wa Lori mkazi wa Tanga na Hassani Abdallah Ramadhani, Utingo wa Lori mwenye Hati ya kusafiria Na. TAE667038 mkazi wa Muheza, Tanga.
Aidha, imefafanua kuwa miili ya Marehemu hao imetambuliwa na ndugu zao isipokuwa marehemu wawili, ambao ni Said Mohamed Dige na Peter Blass Munishi huku ndugu wa marehemu wakihimizwa kufika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutambua miili ya wapendwa wao.
from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/DAnlqv4
via IFTTT
Comments
Post a Comment