Edo Kumwembe Afunguka Kwanini Fei Toto Asifiwi Kwa Kiwango Chake Uwanjani Kama Anavyosifiwa Pacome


Feisal Salum Vs Edo Kumwembe

Ameandika Edo Kumwembe:

Hata hivyo, Fei haimbwi. Hakuna anayepiga kelele. Kwanini aimbwe wakati anacheza Azam? Kuna wachezaji wanafunga mabao mazuri lakini kwa sababu hawapo Simba na Yanga basi hatuwapigii sana kelele na wala mabao yao hatuyaposti mitandaoni kwa mbwembwe kama mabao ya kina Pacome Zouzoua.

Kama Feisal angekwenda Simba basi kiwango hiki hiki ambacho kinatumika na Wanayanga kumsifu Pacome ndicho kiwango kile kile ambacho watu wa Simba wangekuwa wanamsifu Fei. Tatizo kubwa Fei amekwenda katika klabu ambayo haina mashabiki wengi kama wa Simba na Yanga. Amekwenda katika klabu ambayo nadhani hata wachezaji wa kigeni hawapewi sifa wanazostahili.

Naamini hata kina Kipre Tchetche hawakupewa sifa wanazostahili kwa sababu walikuwa Azam. Vipi kuhusu James Akaminko? Unadhani anaweza kusifiwa kama ambavyo Mudathir Yahya anasifiwa pale Jangwani? Hapana. Mpira wetu una utamaduni wake.” 😃

— Edo Kumwembe.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/OoqW8lR
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI