Makonda afichua siri Mbowe kwenda Ikulu alipotoka gerezani




Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Paul Makonda ameeleza kuwa, kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kwenda Ikulu alipotoka gerezani kilikuwa na maana halisi ya dhamira ya kukuza demokrasia ya Rais Samia Hassan.

"Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt. Samia anafanya kazi kwa msaada mkubwa we Mwenyezi Mungu katika kuongoza Taifa hili na ukitaka kujua hilo dalili mojawapo ya mtu anayeaaidia ni Mungu ni kuwa na Upatanishi"

"Rais Samia alianza kuwapatanisha Watanzania bila kujali itikadi ya vyama vyao, kabilabwala kipato na kila aliyepeleka malalamiko alimsikiliza na kuchukua hatua"

"Mbunge wenu wa zamani hapa Hai hata sura yake imebadilika sababu ndani yake anajua Rais Samia ametumwa na Mungu na nanjua wengine watakebehi na kutoa tafsiri nyingi lakini jiulizeni swali moja...anayepanga ratiba za binadamu ni nani? Maana yake Mungu alishampanga Samia kuwa Rais"

"Mbowe katika mahabusu stendi yake ya kwanza kafikia Ikulu na alipotoka alieleza na kukiri kuwa dhamira ya maridhiano Dkt. Samia ni dhamira njema...halafu mtu huyohuyo anakuja tena kusema hakuna maridhiano na bado anapiga simu kwa Rais Samia kuomba michango na anapewa."




from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/VjxOktF
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI