Simba Yafichua Bilioni za Mo Dewji




Simba imefichua kuwa mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'MO' alichangia Sh2.4 bilioni katika bajeti klabu hiyo kwa msimu wa 2022/2023.

Akitoa taarifa ya fedha ya klabu hiyo ya 2022/2023, Mhasibu wa Simba, Suleiman Kahumbu amesema awali walipanga kukusanya Sh12.3 bilioni kwa msimu huo na mchango wa MO ulichangia kwa kiasi kikubwa wakavula lengo hadi Sh15 bilioni.

“Katika bajeti ya fedha ya msimu wa 2022/23 rais wa heshima wa Simba Mohamed Deji alituchangia kiasi cha Sh2.4 bilioni, fedha ambazo zilienda moja kwa moja kwenye kufanikisha kukusanya bilioni 15 ambazo zimetupa faida kwa kiasi kikubwa," amesema Kahumbu.

Kahumbu amesema hayo Leo januari 21, 2024 katika mkutano wa mwaka wa klabu hiyo unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Dar es Salaam.



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/0wHxcug
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI