Tutawapima Wabunge, Madiwani kwa Kazi na sio Maneno - Paul Makonda

 

Tutawapima Wabunge, Madiwani kwa Kazi na sio Maneno - Paul Makonda

Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda, leo Januari 19,2024 ameanza ziara yake kwa kuongea na Wakazi wa Tegeta Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema Wabunge, Wawakilishi na Madiwani watapimwa kwa kazi wanazofanya na sio kwa maneno au kujipendekeza kwa Viongozi ambapo amesemaa wasiofanya kazi taarifa zao zitapelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM (Rais Dkt. Samia), kwamba hawafai kupewa nafasi ya kugombea tena mwaka 2025.


Makonda amenukuliwa akisema;


“Duniani kote hawajawahi kumaliza matatizo hata Mataifa makubwa tunayokimbilia kuyaomba bado yana changamoto, nilikuwa namsikia Rais wa Marekani anajadili jinsi gani wanataka kujenga barabara na madaraja kwenye Nchi yao Marekani nao wapo kwenye ujenzi wa barabara, tafsiri yake ni kwamba changamoto haziwezi ktuisha siku moja, zinaendelea kuwepo kutokana na idadi ya watu, mabadiliko ya tabianchi na hali ya kiuchumi, vinginevyo tungeweza kujenga lami kote”


“Mwaka huu 2024 na 2025 tutawapima Wabunge na Wawakilishi na Madiwani namna gani wanatatua changamoto za Wananchi wao na jinsi gani wapo mstari wa mbele kukijenga Chama chao, awamu hii CCM hii ya Dkt. Samia na Mimi nikiwa Msemaji na nimeshasema tangu nakabidhiwa ofisi sitobeba mzigo kila Mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kama hamfanyi kazi ya utekelezaji wa Ilani na kutatua changamoto za Watu, kwa kauli moja tutakupima kwa kazi, sio kwa maneno, sio kwa kugawa kanga kipindi cha uchaguzi na kuwarubuni Wajumbe, sio kwa kujipendekeza kwa Viongozi bali tukienda kwa Wananchi wakasema naam Mbunge wetu ndiye alipambania hii Shulea au Kituo cha Afya kikajengwa kauli hizo ndio zitafanya uteuliwe tena kupeperusha bendera ya CCM”


“Na kwenye ziara kote nitakakopita kama wewe Mbunge haufanyi kazi na hauonekani tunayo Timu ya kutosha kuchukua taarifa tutampelekea taarifa Mwenyekiti, kwamba Mwenyekiti tukienda na huyu tunapigwaa”



from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/qeDykYS
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI