Posts

TCRA yatoa sababu bando kwisha haraka

Image
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuongezeka kwa mitandao ya simu na kasi ya simu janja nchini ni miongoni mwa mambo yanayochangia ‘bando’ kwisha haraka.  Mkurugenzi wa Masuala ya Sekta wa TCRA, Dk. Emmanuel Manasseh, aliyasema hayo jana mkoani Dar es Salaam, wakati wa mkutano wake na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF). Alitaja mambo mengine yanayosababisha kumaliza 'bando' kwa haraka kuwa ni kuongezeka kwa kasi ya mtandao kwenye simu janja mfano kutoka 3G hadi 4G. Mambo mengine, kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ni ubora wa video na picha unavyoongezeka unasababisha matumizi nayo kuongezeka. "Tuna “application” mbalimbali kwenye whatssap zinafanyiwa ‘update’ mara kwa mara nazo zinatumia data. Watumiaji wengi wa simu kuna vitu vinaendelea kwenye simu yake lakini mtumiaji hajui. Uwapo wa ‘application’ nyingi, zingine hazitumii hivyo zinamaliza ‘bando’,” alisema.   Alisema mamlaka hiyo imekuwa ikifanya majaribio mbalimbali ili kuhakikisha watoa huduma ...

Shalo Mwamba, Mpoto na Sarafina Kimenoga Dubai....

Image
Wasanii kutoka Tanzania, Sholo Mwamba na Sarafina leo wameutambulisha muziki wa Tanzania katika jukwaa jingine la kimataifa walipofanya shoo kwenye ukumbi wa Sea Plaza katikati ya eneo la Dubai Expo. Watu wa mataifa mbalimbali wakiwa wamesubiria shoo hiyo iloyochelewa kuanza kwa sababu za kiufundi, Sarafina ndiye alikuwa wa kwanza kupanda stejini na kuimba na kucheza huku akiwashirikisha mashabiki kutoka mataifa mbalimbali kwa kuimba huku akiwaeleza kisa cha hadithi ya kila wimbo aliouimba. Safari ya kuitangaza Tanzania ilikolea zaidi alipopanda stejini msanii wa Singeli Sholo Mwamba na kuonekana kuwachezesha watu wa mataifa mbalimbali. “Tumekuja hapa Dubai kutumia sanaa na utamaduni wetu kuitangaza Tanzania. Leo dunia imejua Tanzania kuna singeli na kuna muziki mzuri, usiku huu Sarafina amepata shoo nyingine katika ukumbi wa Earth Stage na kesho kazi inaendelea ukumbi mwingine uitwao Sun Stage ambapo Sholo Mwamba na Mrisho Mpoto watafanya shoo nyingine kubwa. Ni wiki ya san...

Mange Kimambi Afunguka "Msameheni tu Diamond, Yeye na Team yake Hawakujua Maana ya Ile Bendera Ila Ajipange"

Image
Ameandika Mange Kimambi "Naona wengi mmetaka ni -address hili swala la confederate flag kwenye video mpya ya Diamond, mi naona tumsamehe tu. Mi nimemuonea huruma tu maana nimeona ni kwamba tu hakujua maana ya hiyo confederate flag. Unless kama mtu alisoma historia ya utumwa especially kwa upande wa marekani au unless ana exposure sidhani kama anaweza kujua hii bendera ina maana gani. Obviously hata wanaomzunguka hawana exposure vile vile kwa hiyo hakuna aliejua maana ya hiyo bendera. Ila kuna siku lazma atajikuta anaulizwa kuhusu hili akiwa nchi za nje hususan marekani. Maana marekani hawana mchezo kabisa kwenye swala la hii bendera. So cha kufanya ni ajipange tu siku akiulizwa atajibu nini, maana kama kuna siku atafanya interview marekani piga ua hii issue lazma watamkalia nayo kooni mpaka aombe msamaha . Hawatomwelewa mpaka aombe msamaha. Wamarekani weusi wako too sensitive na issue ya hii bendera… Ila kwa sisi watanzania tumsamehe tu maana naamini kama angejua maana yak...

Adebayor kuvunjiwa benki Simba, waifuata Berkane

Image
BAADA ya kulazimisha sare ugenini juzi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, jana saa 12:00 jioni kwa saa za Niger ambazo ni sawa na saa 2:00 usiku kwa Afrika Mashariki, wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa kwa ngazi ya klabu, Simba walikwea pipa juu kwa juu .... juu kuelekea nchini Morocco tayari kwa mchezo unaofuata dhidi ya RS Berkane. Simba juzi iliondoka na pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Union Sportive Gendarmerie Nationale (USGN) hiyo ikiwa mechi yake ya pili na ya kwanza ugenini kwenye hatua ya makundi, hivyo kukaa kileleni mwa Kundi D ikiwa na alama nne kutokana na kushinda 3-1 katika mechi ya kwanza nyumbani dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast ambayo juzi nayo ilitoa kipigo kama hicho ikiwa kwao dhidi ya RS Berkane. Katika mchezo wa juzi, winga wa Union Sportive Gendarmerie Nationale, Victorien Adebayor, ambaye alionyesha kiwango cha hali ya juu alihusishwa na kutua Msimbazi msimu ujao, mwenyewe akisema hawezi kuka...

Jamhuri "Sabaya Alitumia Silaha Kupora"

Image
WAKILI wa wajibu rufani kwenye kesi ya jinai namba 105, Ofmedy Mtenga, amedai mahakamani kuwa silaha zilitumika katika tukio la kupora fedha na mali nyingine katika tukio linalodaiwa kufanywa na Lengai Ole Sabaya kwenye duka la Mohamed Saad, lililoko Mtaa wa Bondeni jijini Arusha. Wakili huyo alitoa madai hayo jana wakati wa usikilizwaji wa Rufani namba 129, katika shauri lililokuwa linamkabili, Ole Sabaya na wenzake wawili, mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sedekia Kisanya. Akijibu hoja ya saba ya mawakili wa waleta kwa nini wateja wao walistahili kutiwa hatiani na kufungwa miaka 30 kwenda jela, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mtenga, alidai kwamba kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na mashahidi wa mashtaka katika tukio hilo kulikuwapo na silaha. Alidai kwamba kwa mujibu wa shahidi wa sita wa mashtaka Bakari Msangi, kwenye kielelezo cha kwanza walichokitoa mahakamani cha maelezo aliyoandika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, silaha zinaonekana kutumika katika tukio la ...

Huyu ndiye Aliyemuoa Diva Loveness Mtangazaji wa Wasafi

Image
USIKU Waopendanao duniani, Valentine’s Day 2022; muda wa saa mbili usiku, mtangazaji wa Wasafi, Diva Gissele Malinzi au Diva The Bawse alidai kufunga ndoa ya Kiislam na mwanamue aliyefahamika kwa jina la Abdul. Mrembo huyo alitoa taarifa za ndoa yake hiyo katika kipindi chake cha Lavidavi na kudai kuwa, aliamua kufunga ndoa ya siri na kijana huyo kwa sababu ndiye mtu aliyekuwa akimtaka. “Usiku wa Valentine, muda wa saa mbili usiku, nilifunga ndoa na mume wangu, Abdul na ndoa hiyo ilihudhuriwa na watu wasiozidi kumi, kwa sababu nilitaka iwe hivyo, lakini sasa hivi tupo kwenye maandalizi ya kufanya sherehe kubwa ya ndoa yangu,” alisema Diva. Hata hivyo, swali la wengi limekuwa ni juu ya mwanaume huyo ni nani hasa? Katika kuchimba, Gazeti la IJUMAA limebaini kuwa, mwanaume huyo anaitwa Abdulrazak Salum na alijipatia umaarufu mkubwa mitandaoni kutokana na video zake anazojirekodi kwa ajili ya kuelimisha jamii hususan wapendanao na namna ya kuishi vizuri na mwanamke au mwanaume ...

Nape Nhauye "Sasahivi Hatutafunga Vyombo vya Habari, Tutadeal na Mwandishi au Mtangazaji Husika Aliyekosea"

Image
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kupitia Clouds360 ya CloudsTV leo amesema Serikali haina mpango wa kuvifungia Vyombo vya Habari kwa makosa ambayo yamefanywa na Waandishi wao ambapo amesema kwa sasa watakuwa wanatoa adhabu kwa Waandishi wa Habari waliofanya makosa. "Hatuna mpango wa kufungiana Media, kwa mujibu wa sheria ya 2016 ni kukushughulikia wewe uliyeleta shida kama Mwandishi na sio Media, Gazeti lina Wafanyakazi 50 yule Mfagiaji, Mhasibu hausiki na story halafu sisi tuwaadhibu wote haifai, mbona Daktari akikosea hatufungi Hospitali?" ——— Nape Nnauye. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/m5ApZjI via IFTTT