Posts

Mwanafunzi wa Sekondari Pandahill Adaiwa Kupotea Akikimbia Adhabu Shuleni

Image
Ester Noah Mwanyilu, Mwanafunzi wa Kidato cha Tano, Mchepuo wa PCB, Shule ya Sekondari Pandahill hajulikani alipo baada ya kudaiwa kupotea zaidi ya mwezi mmoja uliopita wakati akikimbia adhabu kutoka shuleni hapo Sauti inayodaiwa ni mzazi wa Mwanafunzi mtoto huyo inaeleza kuwa, maelezo hayo yametolewa na Shule husika licha ya kuwa kuna mazingira tatanishi. Pia, inadaiwa kuwa kabla ya kupotea Ester aliandika barua ambayo ndani yake aliandika “Naomba Mwalimu Jimmy aache kuwafanya Wanafunzi kuwa na maisha magumu kama alivyonifanyia mimi.” Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Afisa Elimu Mbeya (Sekondari), Ernest Hinju amesema “Ni tukio la kweli, lipo chini ya Jeshi la Polisi, wanapeleleza na ndio wana majibu lakini bado Mtoto hajapatikana.” from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/IGBfP97 via IFTTT

Maskini...Dili la Kocha Nabi Laekekea Kushindwa South Africa Msimamo Wake Wamponza

Image
Mazungumzo kati ya Kaizer Chiefs na wakala wa Nasreddine Nabi yameripotiwa kufifia huku pande hizo mbili zikijipapatua kutafuta muafaka. Kocha huyo raia wa Tunisia anasemekana kufanya kazi benchi lake la ufundi aliokuwa akifanya nao kazi katika Klabu ya Yanga ambayo inajumuisha kocha msaidizi, kocha wa makipa, na kocha wa mazoezi ya viungo. Hata hivyo, uongozi wa Kaizer Chiefs unadaiwa kugoma kufanya mabadiliko makubwa katika benchi lao la ufundi la sasa ambalo linaongozwa na Arthur Zwane. Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa, mashabiki wengi wa Kaizer wamemtaka Nabi kutokubali masharti ya Glamour Boys, badala yake asimamie msimamo wake kwani iwapo timu inamhitaji kweli basi watakubaliana na matakwa yake. Kaizer Chiefs walikuwa na mkutano wikendi iliyopita na wenye lengo la kutatua suluhu kuhusu vikwazo vya kocha Nabi. Taarifa kutoka chombo kimoja cha habari nchini Afrika Kusini, TimesLIVE kimearifiwa kuwa dili hilo bado si la uhakika, na kwamba Amakhosi wamekuwa wakiw...

Yanga Hawana Uwezo wa Kumlipa Mshahara Simon Msuva Kwa Sasa

Image
Anaandika Mchambuzi @boiboimkali ✍️ "Simon Msuva alikuwa ankusanya Mshahara wa kiasi cha Dola 12000 kwa wiki ambazo ni sawa na kiasi cha Shilingi Milioni 28 za Kitanzania, Kwa ujumla kwa mwezi akusanya Dola 50,000 Ambazo ni sawa na kiasi cha shillingi Milioni 117 za kitanzania" "klabu ya Yanga imekuwa ikihusishwa na kumsajili Simoni Msuva kutokana na Mchezaji huyo kumaliza kwa Mkataba wake na klabu yake ya Al Qadasiah ya nchini ya Saud Arabia" from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/UOrkq3I via IFTTT

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa awatoa hofu watanzania kuhusu Bandari ya DSM

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewahakikishia Watanzania kwamba Serikali haitodharau maoni na ushauri wanaoutoa kuhusu maeneo yenye hofu kwenye mradi wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam. Waziri Mkuu Majaliwa amewataka pia Watanzania waendelee kuwa na imani na Serikali pamoja na wawakilishi wao ndani ya Bunge kwani Serikali imejidhatiti kuhakikisha bandari inakuwa na ufanisi unaoendana na mahitaji ya sasa na kwa kuzingatia manufaa ya kijiografia ya Nchi yetu. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumanne, Juni 20, 2023 katika sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya chuo cha International Evangelism Centre kilichoko Sakila jijini Arusha ambapo amesema bandari haijauzwa, bali Serikali inataka kubadilisha Muwekezaji ili iweze kuendeshwa kwa ufanisi na tija zaidi. Majaliwa amesema wakati wa kuingia mikataba utakapofika Wataalamu wa uchumi nchini wataishauri Serikali kuhusu muda wa uendeshaji wa uwekezaji huo, hivyo amewataka Wananchi waendelee kuwa na subra. from UDAKU SPECIAL https:...

Serikali yashauriwa kutoruhusu safari za mabasi usiku

Image
Serikali imeshauria kusitisha utaratibu wa mabasi kusafiri usiku kutokana na uwepo wa hatari kubwa ya kusababisha majanga kwa sababu madereva wanaoendesha magari usiku huwa hawalali mchana, badala yake huwa wanafanya kazi nyingine. Ushauri huo umetolewa bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa Bukoba Vijijini, Dkt. Jasson Rweikiza ambapo amesema kuwa safari za usiku ni hatari na bado hakuna na uwezo wa kudhibiti magari yanayosafiri usiku. Amesema kuwa mwaka 1987 alikuwa akifantya kazi Serikali za Mitaa mkoani Dodoma na familia yake ilikuwa ikiishi Dar es Salaam, hivyo mara nyingi alikuwa akisafiri usiku na kwamba vitu alivyokuwa akiviona barabarani ni vibaya sana. “Usafiri wa usiku sio mzuri. Hatujaweza kudhibiti madereva wetu kuwa na nidhamu ya kulala mchana, wasafiri usiku. Mchana wanafanya kazi nyingine za kubangaiza, usiku wanaendesha gari, ajali zilikuwa ni nyingi sana,” amesema Rweikiza Amesema kutokana na hali hiyo, aliyekuwa Waziri Mkuu mwaka 1994, John Malecela alisitisha ...

Baada ya Kula Tunda Kinyemela Kwa Muda Mrefu Bahati Aamua Kumuoa Diana Marua

Image
Africa music wonder kid, Kelvin Kioko Bahati (@bahatikenya) amemchumbia Diana Marua kwa mara ya pili, atangaza rasmi tarehe ya harusi na mpenzi wake huyo wa muda mrefu. Mkali huyo kutoka Kenya ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa habari hii njema kwa kuandika; "Amesema ndio, rasmi na tangaza kuwa Disemba 12,2023 itakuwa siku yetu ya harusi". Muda mfupi baadae @diana_marua nae alitoa shukrani zake za dhati kwa Baby Daddy wake huyo kwa upendo na thamani anayo mwonesha. Mwaka 2017, mwezi Oktoba taarifa zilienea kuwa msanii huyo amefunga ndoa na Diana kimya kimya na baada ya mazungumzo na MondayBlues, Bahati alisema tukio hilo lilikuwa la Kifamilia na linajulikana kama ruracio na sio harusi kamili, kama watu walivyodhani. Msanii huyo wa zamani wa muziki wa Injili ana watoto watano, ambapo watatu wa kuwazaa Diana na wengine wa wawili aliwa-adopt kutoka kituo cha Watoto cha ABC kama sehemu ya kurudisha kwa jamii. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/lZ6MawX via IFTTT...

Hatimaye Diamond Platnumz Amkumbuka Lava Lava.....

Image
Subira huvuta kheri, ndio pengine methali ambayo wengi wanahisi inamfaa msanii wa muda mrefu ndani ya lebo ya Wasafi WCB, Lavalava. Msanii huyo katika miaka ya hivi karibuni ametoweka machoni pa mashabiki wa muziki, licha ya kujisatiti na kujitahidi kuachia miziki kila mara, lakini miziki yake imekuwa ikiishia kwenye paa za studio za Wasafi tu! Wengi walimsahau kama alikuwepo, kiasi kwamba hata bosi wake Diamond Platnumz kuonekana kumsahau kama alikuwa msanii mwenye mkataba chini ya lebo yake. Diamond aliwekeza nguvu zake nyingi katika promo za wasanii Zuchu na Mbosso ambao kwa sasa wanafanay vizuri, lakini kwa muda hakuwahi kuonekana akifanya udhubutu wa kusukuma kazi za Sanaa za Lavalava, kama ambavyo imekuwa kawaida yake tangu enzi za msanii wake wa kwanza – Harmonize. Lakini baada ya Lavalava kuachia kibao chake kipya hivi majuzi kinachokwenda kwa jina ‘Tajiri’, bosi wake aliguswa na mapenzi tena, na kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kumpiga promo hatari Lavalava kwa ...