Wajawazito wabebwa kwenye matenga kwenda hospitali Tunduru
Baadhi ya wananchi katika kijiji cha Mpanji wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma,wamelalamika kukosa zahanati katika kijiji hicho huku akina mama wajawazito wakilazimika kuwekwa kwenye matenga ya nyanya na kupakizwa kwenye pikipiki kupelekwa hospitali ya misheni ya Mbesa kilomita zaidi ya 35 hali ambayo wamedai inahatarisha usalama wa maisha yao.
Wakitoa malalamiko hayo kwa mkuu wa wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma,Bw.Juma Homera, wananchi hao wamesema tangu nchi ya Tanzania ipate uhuru hawajawahi kuwa na zahanati,hali hiyo huwalazimu akina mama wajawazito kuwekwa katika matenga ya nyanya na kupakiwa kwenye pikipiki kwenda hospitali ya misheni ya Mbesa wilayani humo kilomita zaidi ya 35.
Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya ya Tunduru, Bw.Homera akasikitishwa na kasi ndogo ya viongozi wa kijiji hicho kuhimiza ujenzi wa zahanati huku akiwapa miezi minne kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa zahanati hiyo ili halmashauri iweze kutoa vifaa vya kiwandani na yeye mwenyewe akiahidi kutoa mifuko 78 ya saruji.
from Utundu kitandani http://bit.ly/2XNRm9Y
via IFTTT
Comments
Post a Comment