Maktaba ya Kisasa Kujengwa Lupaso
Maktaba ya kisasa kujengwa katika shule ya msingi Lupaso ambayo amesoma Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa ili kumuenzi kiongozi huyo.
Mkuu wa shule hiyo, Charles Maduhu amesema kuwa uongozi wa shule hiyo umeahidi kujenga maktaba ya kisasa ambapo amesema katika makaba hiyo moja ya kitabu ambacho lazima kitawekwa ndani ni My life my Purpose (Maisha yangu Kusudio langu)
Kwa mujibu wa gazeti la Nipashe Mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema kuwa tayari fadha wanazo za kuanza kujenga maktaba hiyo ya kisasa.
Aidha amesema kutokana na kitabu hicho kuwa na mambo mengi aliyoyaandika Rais wa awamu ya tatu mazuri kwa taifa hivyo hata watoto wanaosoma katika shule hiyo wakiweza kupata fursa ya kuyasoma watapata cha kujifunza kutoka kwake.
Naye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu amesema halmashauri itahakikisha shule hiyo inaenziwa kwa mambo mbalimbali ikiwemo uboreshajiwa madarasa pamoja na miundominu mingine ili kumuenzi Mkapa.
from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/317osVF
via IFTTT
Comments
Post a Comment