Sri Lanka wapiga kura ya ubunge
Raia nchini Sri Lanka wanamiminika vituoni hivi leo kwa ajili ya uchaguzi wa bunge unaotazamiwa kuimarisha nguvu za Rais Gotabaya Rajapaksa madarakani.
Wakati vyama vya upinzani vikitumia kampeni yao kupigania nafuu ya maisha kutokana na hali mbaya ya uchumi iliyosababishwa na janga la COVID-19, chama cha Rais Rajapaksa kimetumia kaulimbiu ya "serikali yenye nguvu zaidi" ili kumuwezesha kutimiza ahadi alizozitowa wakati akiwania urais.
Chama hicho kinataka ushindi wa thuluthi tatu ili kilidhibiti bunge na kiweze kubadilisha katiba na kurejesha madaraka ya rais, ambayo kinasema yalitwaliwa kwenye mabadiliko ya katiba ya mwaka 2015.
Zaidi ya raia milioni 16 wana haki ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa leo, kuchaguwa wabunge 196 kati ya 225, ambapo wabunge waliosalia hupatikana kutokana na mgawo wa kura za jumla kwa kila chama ama wagombea huru.
Miongoni mwa wagombea mashuhuri ni rais wa zamani na kaka wa rais wa sasa, Mahinda Rajapaksa, anayeshindana na Sajith Premadasa, mtoto wa rais mwenzake wa zamani aliyeuawa na waasi mwaka 1993, Ranasinghe Pramadasa.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/30s06XD
via IFTTT
Comments
Post a Comment