Kumekucha Zuchu Rayvanny na Zuchu




ACHANA na rekodi za wimbo wao wa Number One unaendelea kukiamsha mitaani na mtandaoni, lakini habari nzito ni kwamba eti kuna kitu kinaendelea kati ya memba wawili wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na Zuhura Othman ‘Zuchu’

Ukaribu wenye shaka na viulizo kati ya Rayvanny na Zuchu umeendelea kuzua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ya ndani na nje ya Bongo.

Wajuzi wa mambo wanasema kwamba, ukitazama namna ambavyo Zuchu anajibebisha kwa Rayvanny, hata kipindi kile akihusishwa na bosi wao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’
ilikuwa ni cha mtoto.

 

Taarifa za wawili hao kuhusishwa na ishu za kimapenzi zilianza kuvuma pale Rayvanny kupitia ukurasa
wake Instagram alitundika picha za kimahaba akiwa na Zuchu kisha  akaandika; “Penzi limetaradadi… tangu hapo stori zao za madai ya kwamba wanatoka kimapenzi, zimeendelea kuwa ni nyingi mno.

Baadhi ya watu wa familia hiyo kubwa ya Wasafi wamekuwa wakishabikia ukaribu huo kuanzia Director Kenny, Baba Levo na hata Esma Khan ambao wamekuwa wakidai mambo yawekwe hadharani na ubwabwa uliwe.

 

Katika mahojiano yake na kituo kimoja cha runinga kule Kahama hivi karibuni, Zuchu aligoma kujibu swali hilo na kuishia kucheka, jambo linalozua hisia kwamba huwenda walifanya hivyo kwa lengo la kuupa promo wimbo wao huo wa Number One.

Hadi jana, wimbo wao huo ulikuwa umetazamwa mara zaidi ya milioni 2.5 pale mjini YouTube katika kipindi
cha wiki moja.




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3oqa58X
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI