Ahmed Ally wa Simba Amekubali Yaishe "Gape Limekuwa Kubwa Sana"



Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC ni kama wamekata tamaa ya kutetea ubingwa msimu huu 2021, baada ya kushindwa kumfunga Young Africans jana Jumamosi (April 30), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Pambano hilo lilisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Soka la Bongo na nchi jirani, lilimaliza dakika 90, kwa Manguli hao kugawana alama, kufuatia sare ya bila kufungana.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amekiri Gape la alama limekua kubwa sana kati yao na Young Africans, licha ya kubakiwa na michezo mingi kabla ya msimu huu kukamilika.

Amesema wanachokiangalia kwa sasa Simba SC, ni kuhakikisha wanashinda michezo yao yote ili kufanikisha jukumu la kupata alama zote, na ikitokea mpinzani wao (Young Africans) anapoteza itakua ni faraja kwao.


“Mbio za Ubingwa kwetu Simba SC zinakuwa ngumu kwa kuwa Mpinzani wetu anaendelea kukusanya pointi nyingi.”

“Sisi tutapambana kushinda mechi zetu tuone mwisho wa msimu itakuaje lakini uhalisia ni kwamba gape limekuwa kubwa.” amesema Ahmed Ally.

Simba SC imefikisha alama 42 baada ya matokeo ya jana dhidi ya Young Africans inayoendelea kuongoza Ligi kwa kuwa na alama 55.


from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/AIHlcWb
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI