Posts

EFM Radio Yazidi Kukimbiwa na Watangazaji, B Dozen na Oscar Oscar nao Wamesepa

Image
Ameandika Majizzo: Ilikuwa wakati mzuri sana kufanya kazi na ndugu zangu Maulid Kitenge, Gerald Hando, B Dozen na Oscar Oscar. Nitaendelea kuwashukuru na kuwaheshimu sana kwa mchango walioweka hapa #EFMnaTVE. Nawatakia mafanikio katika ajira zao mpya, mafanikio yao ni mafanikio ya tasnia na hiyo ni furaha yangu. . All the best ndugu zangu🙏🏻 from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/ly82rEm via IFTTT

Hiki hapa kikosi Cha Yanga kitakacho Anza Leo dhidi ya Rivers United

Image
1:Djugui Diarra 2:Djuma Shaban 3:Joyce Lomalisa 4:Dickson Job 5:Bakari Mwamnyeto (C) 6:Ibrahim Abdallah 7:Farid Mussa 8:Yanick Bangala 9:Fiston Mayele 10:Mudathir Yahya 11:Stephen Aziz Ki Wachezaji wa Akiba 12:Metacha Mnata 13:Kibwana Shomari 14:Khalid Aucho 15:Zawadi Mauya 16:Mudathir Yahya 17:Salum Abubakar 18:Clement Mzize 19:Kennedy Musonda 20:Tuisila Kisinda from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/LW6RrCx via IFTTT

Shambulio la kujitoa mhanga laua na kujeruhi zaidi ya watu 70 Mali.

Image
Watu wasiopungua 10 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika shambulio la bomu karibu na kambi ya kijeshi na uwanja wa ndege katikati mwa Mali. Yacouba Maiga, msemaji wa Gavana wa mkoa wa Mopti amesema, zaidi ya watu 60 walijeruhiwa pia katika shambulio hilo lililotokea kwenye mji wa Sevare ulioko katika mkoa huo mapema jana. Kwa mujibu wa Maiga, mripuko huo uliharibu takribani nyumba 20 katika mji huo. Ameongeza kuwa, kuna jumla ya watu tisa waliofariki na takriban 60 wamejeruhiwa, wote wakiwa raia. Kanali Souleymane Dembele, msemaji wa jeshi la Mali, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba takriban watu 10 waliuawa katika hujuma hiyo. Wakati huohuo, taarifa iliyotolewa na serikali ya Bamako, jana hiyohiyo Jeshi la Mali liliteketeza ngome ya magaidi huko Mourdiah na kuwaangamiza magaidi 60 katika mji wa Boni, ambao nao pia uko katika mkoa wa Mopti. Tangu mwaka 2012, Mali imekabiliwa na machafuko kufuatia kuenea kwa makundi yenye misimamo ya kufur...

Miili ya waliojiua kwa njaa kukutana na Yesu yafikia 14.

Image
Miili 14 zaidi imefukuliwa katika makaburi ya watu wanaoaminika kufariki kwa kufunga kutokana na mafundisho yanayofanana na ya kiibada ya kasisi wa Malindi, Paul Mackenzie katika eneo la Shakahola, Magarini. Hii inafikisha 21 idadi ya miili ambayo imefukuliwa na kitengo cha mauaji, wapelelezi wa DCI na maafisa wengine wa usalama. Miili mitano, inayoaminika kuwa ya watu wa familia moja ilipatikana katika kaburi moja. Katika kaburi jingine, miili mitatu ilipatikana juu ya kila mmoja. “Tulimpata, mwanamume, mwanamke na watoto watatu kwenye kaburi moja,” mpelelezi alisema Kati ya miili iliyofukuliwa, watoto walikuwa wengi ikilinganishwa na watu wazima. Kufikia Ijumaa makaburi 58 yalikuwa yametambuliwa. Timu ya maafisa wapatao 100 wakiongozwa na Mkurugenzi wa kitengo cha Mauaji pamoja na mwanapatholojia, maafisa kutoka DCI, Idara ya uchunguzi, na polisi wa kawaida wanaongoza operesheni hiyo. Wananchi hawakuruhusiwa katika eneo la tukio na waandishi wa habari pia walipew...

Vipo vyanzo vingi vya mvi lkn baadhi ni KUCHOKA KWA HOMONI, DAWA KALI, UMRI, KURITHI N.K

Kwa mara ya kwanza Kajala afunguka sababu za kuachana na Harmonize, aibua mapya

Image
NI Mwigizaji Kajala Masanja ambae kwasasa yuko nchini Kenya amefanya mahojiano na Redio Citizen FM ameweka wazi sababu ya kuachana na Staa wa Bongo Fleva, Harmonize. “Ni mazoea mtu akishakuzoea Sana, anakuchukulia poa. Simlaumu yeye ni kijana mdogo, pengine alihitaji ‘space’ manake kuwa na mimi muda tulikuwa pamoja tunafuatana" Alisema Kajala from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/xbcThQy via IFTTT

Sakata Mtoto Aliyezaliwa Kugeuka Kuwa Jiwe..Uchunguzi Wabainisha Haya

Image
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt.Khalfany Haule amesema taarifa ya uchunguzi iliyofanywa kuhusu sakata la Mtoto kugeuka jiwe Musoma imethibitisha bila shaka kuwa hakuna aliyezaa jiwe wala hakuna Mtoto aliyegeuka jiwe bali Amina Abdallah aliyemuahidi kumzalia Hamis Mtoto wa kiume kisha akamzalia wa kike aliamua kuokota jiwe na kulipeleka kwa Wakwe na kuzusha alizaa Mapacha lakini Mtoto wa kiume amegeuka jiwe huku akitaka lizikwe haraka kuondoa mikosi. DC Haule amesema “Amina Mkazi wa Katoro Chato alihamia kijiji cha Mwabuki Bariadi akiuza pombe za kienyeji, kuhudumia vinywaji Bar na uhudumu wa Gesti, tarehe 27/3/2023 alijifungua Mtoto wa kike Zahanati ya Mwabuki akiwa ni Mtoto wake wa tatu aliozaa na wanaume tofauti (Kila Mtoto na Baba yake), Mtoto huyu alizaa na Hamisi mwenye Makazi yake Mungaranjabo, Buhare hapa Musoma, Amina alimuahidi kumzalia Mtoto wa kiume Hamisi lakini kwa bahati mbaya Mtoto aliyezaliwa alikuwa wa kike” “Hamisi yupo Dar na alituma nauli ili Watoto wapelekwe kwa...