TAARIFA: Wachezaji wa Simba watakao ukosa mchezo wa Power Dynamos ligi ya Mabingwa
TAARIFA: Wachezaji wa Simba watakao ukosa mchezo wa Power Dynamos ligi ya Mabingwa Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema wachezaji watatu wataukosa mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamo Mchezo huo utapigwa Jumapili, Oktoba 1 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi Ahmed amesema beki Hennock Inonga bado anaendelea kuuguza jeraha alilopata katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji Ahmed pia amewataja mlinda lango Aishi Manula ambaye bado anaendelea kuimarika wakati Aubin Kramo hayuko tayari kutumika kwenye mechi ya ushindani kwani kuwa bado hajapona sawasawa majerah "Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki timu ilirejea mazoezini jana kujiandaa na mchezo dhidi ya Power Dynamos" "Mpaka sasa ni wachezaji watatu (Inonga, Kramo, Manula) ambao tuna uhakika wataukosa mchezo lakini wachezaji wengine wote wanaendelea na maandalizi" "Tunatarajia kucheza mechi moja ya kira...