Njia 9 Za Kutumia Kumtongoza Mwanamke Ambaye Hamko Ligi Moja
Kutongoza mwanamke aina hii kunaogofya baadhi ya wanaume. Wengi husema kuwa kuaproach mwanamke wa kawaida ni rahisi lakini ikija kwa kutongoza mwanamke ambaye yuko ligi nyingine kunawatia baridi. Huyu ni mwanamke ambaye akiingia mahali kila kitu kinasimama na kumuangalia yeye. Kila akipita watu wanamkodolea macho ya kuingiwa na tamaa. Kila anapotembea unajiskia dunia yote ikikuzunguka kichwani. Kiufupi ni mwanamke mrembo unayemzimia kiasi cha kuwa unashindwa kumtongoza. Kama wanaume wengine, unashindwa kumtongoza kwa sababu anaoneka level nyingine, anaonekana tofauti kabisa na mwanamke wa kawaida. So utafanya nini ili kumpata mwanamke kama huyu? Usikate tamaa kwani kama mwanaume yeyote, pia wewe una nafasi bora ya kumpata mwanamke huyu na kumfanya wako kabisa. Ujanja wa kufuata ni kama ifuatayo. Zifuatazo ni jinsi ya kutongoza mwanamke aina hii: #1 Kuwa na sababa za uhakika. Kabla kuanza chochote, unafaa kujiuliza kwa nini unataka kumtongoza huyo mwanamke. Najua hautak...