Watoto wa Manara, Baba Levo watoboa matokeo Kidato cha Nne
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2023, yakionyesha kuongezeka kwa ufaulu wa watahiniwa kwa asilimia 0.87 na ufaulu wa hisabati ukipanda kuliko masomo yote. Mbali na kuongeza kwa kiwango cha ufaulu, ubora wa ufaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu nacho kimeongezeka kwa asilimia 0.47 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2022. Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Necta Dk Said Mohamed amesema asilimia 37.42 ya watahiniwa wamepata daraja la kwanza hadi la tatu ikilinganishwa na asilimia 36.95 waliopata madaraja hayo mwaka 2022. “Jumla ya watahiniwa wa shule 471,427 kati ya 527,576 wenye matokeo ambao ni sawa na asilimia 89.36 wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza hadi la nne. Waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ni asilimia 37.42,” amesema Dk Mohamed. Kwenye matokeo hayo wapo watoto wa watu maarufu akiwemo Msemaji wa Yanga, Haji Manara ambaye kupitia mtandao wa I