ZISOME HAPA FAIDA ZA KUMSIFIA MPENZI WAKO
Kuna mengi mazuri ambayo huenda mpenzi wako aliwahi kukufanyia, je uliwahi kumshukuru kwa kukufanya ufarijike? Naamini Mungu amekujaalia kuwa na mpenzi mzuri, mwenye kila sifa ambayo ulitamani awe nayo, je ulishawahi kumsifia hata kwa kumwambia ni mzuri? Huenda ulishawahi kufanya hivyo lakini kwa taarifa yako wapo ambao wanahisi kufanya hivyo eti ni ulimbukeni. Ulimbukeni? Kumsifia mpenzi wako unaona ni ulimbukeni wakati wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, wanawake ni watu wanaopenda kusifiwa sana hata kwa madogo wanayoyafanya. Unaona hatari gani kumsifia mpenzi wako kuwa ni mzuri? Unadhani unatumia nguvu gani kumsifia mpenzi wako kutokana na mahaba mazito anayokupatia? Kwa taarifa yako unaweza kuona ni kitu kidogo sana lakini madhara yake kwenye penzi ni makubwa. Kumsifia mpenzi wako kwa yale anayokufanyia kuna faida nyingi sana lakini kwa leo nitagusia chache. Kwanza kunaongeza mapenzi. Mume/mke anaposifiwa kuwa anajua mapenzi hata kama si kwa kiwango kikubwa, anaf...