Kufungwa Kwa Bar ya Last Minute ..Irene Uwoya Adaiwa Kufulia, Vyuma Vimekaza
VYUMA vimekaza! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwanamama na staa wa fi lamu za Kibongo, Irene Uwoya, kufunga baa yake ya Last Minute iliyopo Sinza, Dar, huku sababu zikiwa hazijulikani. Baa hiyo ambayo mbali na kazi yake ya fi lamu, ndiyo ilikuwa ikimuingizia kipato na kumpa jeuri mjini hapa mwanamama huyo, ilifungwa huku taarifa nyingi zilikuwa zikisambaa zikianisha sababu za kufungwa kwa baa hiyo. VYANZO VINASEMAJE Taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali zimesema kuwa, msanii huyo alikosa mtaji wa kuendesha biashara yake na ndiyo sababu akaamua kuifunga. “Hana lolote zaidi ya kufulia na kukosa mtaji wa biashara japo anafi cha tu,’’ kilisema chanzo kimoja kilichoomba kuhifadhiwa jina lake. Haikuishia hapo mmoja wa watu wake wa karibu na Uwoya ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, aliliambia Gazeti la Amani kuwa, Uwoya kakosa kodi ya kulipia pango na hata kwenye mapato ya serikali na ndiyo maana akaamua kuifunga. “Sababu kubwa ya Uwoya kuifunga hiyo baa ni kutokana n...