Posts

Showing posts from March, 2022

Zaidi ya tiketi 800,000 zauzwa mpaka sasa kwa Kombe la Dunia Qatar

Image
  Mashabiki wa kandanda wamenunua tiketi 804,186 za mechi za Kombe la Dunia nchini Qatar baadae mwaka huu katika awamu ya kwanza ya uuzajii.  Shirikisho la kandanda Duniani na waandalizi wa kinyang'anyiro hicho FIFA wamesema wanunuzi wengiwa tiketi hizo wametokea Qatar, Marekani, England, Mexico, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, India, Brazil, Argentina na Saudi Arabia.  Tiketi za mechi ya ufunguzi mnamo Novemba 21 -- ambayo itaihusisha wenyeji Qatar -- pamoja na fainali ya Desemba 18 ndizo zilizonunuliwa kwa wingi.  Timu 32 zitashiriki tamasha hilo na mpaka sasa 27 tayari zimefuzu. Droo ya mwisho ya Kombe la Dunia ambapo timu zitapangwa katika makundi itafanyika Ijumaa Aprili mosi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/biLpmAP via IFTTT

Viongozi Wenye Nguvu Duniani wakubaliana Kutolegeza Msimamo dhidi ya Russia

Image
  Viongozi wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italy, wametoa wito kwa mataifa ya magharibi kutolegeza msimamo wake dhidi ya Russia. Hii ni baada ya Moscow kuonyesha dalili za kupunguza mashambulizi dhidi ya Ukraine katika miji ya Kyiv na miji mingine. Waziri wa mambo ya nje wwa Uturuki Mevlut Cavusoglu, ametangaza kwamba katika mazungumzo ya amani yanayoendelea Istanbul, wajumbe wa Russia na Ukraine wamekubaliana kuhusu badhi ya mambo. Akizungumza na waandishi wa habari mda mfupi baada ya mazungumzo yake ya simu na viongozi wa nchi nne za ulaya ambazo ni washirika wakubwa wa Marekani, rais Joe Biden amesema kwamba wanasubiri kuona kama makubaliano yatafikiwa katika mazungumzo kati ya Russia na Ukraine. Biden amesema kwamba inaonekana kwamba wajumbe katika mazungumzo hayo wamefikia makubaliano kuhusu baadhi ya mambo, lakini kinachosubiriwa ni kuona matokeo ya mazungumzo hayo. "kwa sasa, tutaendelea kutekeleza vikwazo vikali, tutaendelea kutoa msaada wa kijeshi k...

Steve Nyerere "Mimi Sio Msemaji was YANGA, Haji Manara Alitania"

Image
Baada ya Msemaji wa Yanga Haji Manara kumteua Steve Nyerere kuwa Msemaji msaidizi wa klabu hiyo kutokana na kujiuzulu Usemaji wa Wasanii, Steve ameweka wazi kuwa sio kweli kwamba aliteuliwa, ilikuwa ni utani na dongo kutoka kwa Manara. "Haji Manara ni Ndugu yangu mimi na yeye tuna historia kwenye Maisha yetu ya Upambanaji lakini kikubwa Tunataniana sana, Juzi Arusha Aliniwahi kunipa Dongo Hadharani katoa Ajira kwangu Nilifurahi sana Maana ucheshi unaongeza siku za kuishi". "Ikumbukwe kuwa Haji Manara Ni MSEMAJI wa wananchi Timu kubwa katika ukanda wa Africa,...na kikubwa zaidi mimi ni shabiki wa Yanga kindaki ndaki." "Ni Utani, sio kweli mimi MSEMAJI wa Yanga Ulikuwa utani tu kati ya mimi na Ndugu Yangu kaka yangu rafiki yangu.,..,kipenzi HAJI MANARA KING." - Steve Nyerere from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/YGPnXNc via IFTTT

Si Mchezo, Unaambiwa Mgawanyo wa pesa za zawadi Kombe la Dunia upo hivi

Image
Si Mchezo, Unaambiwa Mgawanyo wa pesa za zawadi  Kombe la Dunia upo hivi  from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/P6EaoR5 via IFTTT

WATU Wengi Hawamuelewi NYOKA Ndio Maana Wanapanic ,Chukua Tahadhari Hizi Pindi Uking'atwa

Image
Wengi wakimuona nyoka wanaanza kukimbia ,kupiga makelele.Nani kakuambia kuna nyoka ambaye akimuona mtu anaanza kumkimbiza. Nyoka sio simba au chui ambao tabia zao wakimuona mtu ambaye ni kitoweo kwao wanaanza kumkimbiza kwa nia ya kumla.Kwa nyoka la hasha hakuna nyoka wa aina hiyo awe venomous au non venoumous.Nyoka huwakimbiza rodents tu kama panya sababu ni kitoweo chao. Watu hawamtizami nyoka kama kiumbe wa porini Bali humtizama kama vile kitu kibaya hilo ndio tatizo. Nyoka pekee ni kiumbe namba moja ambaye watu humuelewa sivyo ndivyo Africa,hivyo ni mnyama anayeongoza kuuliwa kikatili Nyoka hupata attention mbaya sababu ya stori ambazo watu husikia pale mtu anapong'atwa Kung'atwa kwingi panatokea pale mtu anapojaribu kumzuru nyoka na kiumbe huyo anajaribu kujitetea Majira ya kiangazi nyoka hujificha sana chini ya mawe,miamba majani au kwenye miti kukaa mbali na joto la jua Mida ya jioni hujitokeza kwa wingi na usiku wakati hali ya joto ipo chini hushamili ...

Hii Hapa Historia Fupi ya Kabila la Wahaya

Image
Wahaya walitokea Afrika Kaskazini na kupitia Uganda na hatimaye kuanza maisha katika eneo la Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania Wahaya ni moja ya makabila yaliyojaliwa wanawake wazuri na wenye maumbo na shepu nzuri pamoja na tabia. Lugha, Tamaduni,chakula (Ndizi) ya watu wa kabila hili inafanana sana na ile ya jamii ya wanyankole wa nchi jirani ya Uganda Wahaya walianza kutambiana toka zamani na kigezo kikubwa ilikuwa ni kuwa na elimu bora “inye nsomile” maana ya “Mimi nimesoma” na huu ukawa mwanzo wa makabila mengine kuwaita “NSHOMILE” Wahaya ni mkusanyiko wa makabila saba,ambayo ni waziba, wahamba wanyambo, wanyaiyangilo, wayoza waendangabo wakala. Ni mkusanyiko kwa maana haya ni makabila kamili sio makabila madogo madogo kama watu wengi wanavyofikiria. Hayo makabila kila moja ilikuwa ni dola kamili iliyokuwa na mamlaka kamili katika nyanja zote za kiutawala,kijamii,kisiasa kiuchumi na kijeshi.Na kila dola lilikuwa na mipaka isiyoingiliana na dola jingine na i...

Ramadhan Kabwili Afichua SIRI nzito Young Africans

Image
  Mlinda Lango Ramadhan Kabwili amevunja ukimya na kueleza kwa undani ukweli wa maisha yake baada ya kushindwa kuonekana kwenye kikosi cha Young Africans msimu huu 2021/22, huku ikielezwa aliachwa mwishoni mwa msimu uliopita. Kabwilia mbaye kwa kipindi kirefu alikua kimya amesema wadau wengi wa Soka la Bongo wamekua hawafahamu kinachoendelea kati yake na Uongozi wa Young Africans, lakini ukweli ni kwamba bado ni mchezaji halali wa klabu hiyo. Mlinda Lango huyo aliyekua sehemu ya kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17 kilichoshiriki Fainali za Afrika 2017 nchini Gabon, amesema ni kweli hayupo kwenye kikosi cha Young Africans kwa muonekano, lakini yupo klabuni hapo na anaendelea kulipwa mshahara wake kila mwezi. “Naomba niweke wazi leo bado nipo Yanga, napokea mshahara wangu kwa wakati na posho kama ilivyo kwa wachezaji wengine,” “Kiukweli nimeamua kuweka wazi kwa sababu sio jambo dogo viongozi wangu wanalifanya, sipo ndani ya timu kwa maana ya kufany...

UCHAMBUZI wa video ya Mtasubiri, DIAMOND na ZUCHU sio siri tena, ni MABUSU na MAHABA ya kutia wivu

Image
  UCHAMBUZI wa video ya Mtasubiri, DIAMOND na ZUCHU sio siri tena, ni MABUSU na MAHABA ya kutia wivu VIDEO: from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/f6MBzWF via IFTTT

Ghana yafuzu Kombe la DUNIA Ikiitoa Nigeria, Vurugu Kubwa Yatokea na Kusababisha Kifo Cha Mtu Mmoja

Image
 VURUGU kubwa ilitokea usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar kati ya Nigeria dhidi ya Ghana. Ubao wa Uwanja wa Moshood Abiola nchini Abuja ulisoma Nigeria 1-1 Ghana na Nigeria kuweza kufungashiwa virago kwa Ghana kupata faida ya bao la ugenini na jumla waliweza kufungana bao 1-1. Baada ya mchezo huo kukamilika mashabiki wa Nigeria maarufu kama Super Eagles walikuwa na hasira kwa timu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki Kombe la Dunia tena wakiwa nyumbani waliweza kushuka moja kwa moja eneo la uwanja. Mashabiki hao walijaribu kuwashambulia wachezaji wa timu ya Taifa ya Ghana na kuharibu baadhi ya miundombinu ya uwanja na kuna video ambayo ilichukuliwa ikionyesha mabomu ya machozi ili kuweza kuwasambaratisha mashabiki hao waliokuwa na hasira kali. Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Ghana ilikuwa ni sare bila kufungana Uwanja Ohene Djan huko Kumasi na Super Eagels waliamini kwamba itakuwa ni rahisi kwa wao kuweza kufuzu jambo amb...

"Naomba Apate Raha, Upendo na Amani" Briana Afichua Sababu za Kutengana na Harmonize

Image
Mlimbwende kutoka Austrialia, Briana Jai amethibitisha kwamba hayupo tena kwenye mahusiano na staa wa Bongo, Harmonize. Akizungumza kupitia kanda ya video ambayo alipakia Instagram, Briana alifichua kwamba imekuwa muda sasa tangu mahusiano yao yalipogonga ukuta. Briana ambaye alikuja kujulika kama mpenzi wa Harmonize mwezi Novemba, mwaka jana amesema vipaumbele vyao maishani vilikosa kuwiana na ndiposa wakaafikiana kutengana. "Mahusiano yetu hatimaye yalikosa kufanikiwa.Nilihisi vipaumbele vya kile tulichotaka na maisha yetu vilikuwa tofauti. Hata hivyo tulikuwa na miezi michache mizuri pamoja. Sitasahau kamwe kumbukumbu tulizoshiriki pamoja na naomba apate raha, upendo na amani. Napeza familia yangu ya Tanzania, nawapenda sana," Briana alisema. Malkia huyo ambaye amekuwa na Harmonize kwa chini ya mwaka mmoja aliweka wazi kuwa kwa sasa yupo nyumbani kwao Australia. Ingawa mahusiano yake na Harmonize yalikosa kufua dafu, Briana ameahidi kuzuru Tanzania katika si...

Vanessa Mdee Awajibu Mashabiki Wanaosema Amezeeka

Image
Mwanamuziki Vanessa Mdee amewajibu mashabiki zake waliokuwa wanamtupia vijembe kwamba amezeeka. Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mdee alisema kwamba kuzeeka ni baraka wala hajutii chochote. "kuna Mtu kasema nishazeeka, kuzeeka ni faraja kwangu hilo sio tusi kabisa wala hata hunitingishi," Mdee alisema. Mdee alishikilia kwamba la muhimu kwa sasa ni kuwa ana furaha katika maisha yake, hivyo kauli za watu hazina madhara yoyote kwake. Baadhi ya mashabiki walisema kwamba tangu kichuna huyo aolewe na Rotimi, ameawiri sana na maisha yake yanazidi kuwa bora. Wengine pia hawakusita kuibua stori za mpenzi wake wa awali, Juma Jux huku Vaessa akisema kwamba hayo ni mambo ya zamani na alishayasahau. Alikuwa anayasema haya wakati akitambulisha rasmi programu yake na mumewe iitwayo Forthebetter.me ambapo shabiki anaweza kujisajili na kulipia kiasi kidogo cha pesa ili kupata burudai, makala mbalimbali, ushauri na kuuliza maswali kuhusu mastaa. from UDAKU SPE...

Siri ya Mti wa ‘Mdigrii’ Kwa Wanafunzi Chuo Kikuu UDSM Mlimani

Image
Ni eneo maarufu na pengine miaka yako ya kuwa chuoni inaweza ikawa na walakini kama hukuwahi kukanyaga eneo hilo. Unaweza usifike hapo, lakini kwa hali ilivyo, lazima ulijue kwa kuwa ni miongoni mwa maeneo machache yanayotajwa kuwa alama muhimu ya chuo hicho. Katika eneo hilo ndipo uliposimama mti mkubwa, ukiwa na matawi makubwa kila upande ukitoa kivuli mwanana kwa wakaao chini yake. Ni mithili ya mabawa ya kuku anapowakumbatia vifaranga. Ni mti uitwao ‘ mdigrii’ uliopo kampasi kuu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Simulizi ya kuvutia Hadithi kuhusu mti huu zinavutia. Haijulikani nani aliupanda, lini na kwa sababu gani, lakini leo umebeba siri kwa jamii ya chuo hicho. Moja ya simulizi mashuhuri kuhusu mti huo ni ile inayodaiwa na baadhi ya wanafunzi kuwa ukisoma katika mti huo, una uhakika wa kuja kuitia kibindoni shahada yako. Mmoja wa wahadhiri chuoni hapo, Dk Dotto Paul, anasema miaka ya 1990 mti huo ulipokuwa mkubwa na ukiwa jirani na ukumbi maarufu wa Nkrumah,...

Kiungo Simba Aitabiria Ubingwa Yanga

Image
WAKATI Ligi Kuu Bara zikibaki takribani mechi 18 kwa kila timu kucheza kumaliza msimu huu, vinara wa ligi hiyo, Yanga SC, wanaonekana kuwa na wakati mzuri wa kuwa mabingwa. Kasi yao katika ligi msimu huu, inawafanya wengi waamini hivyo kwani ndiyo timu pekee hadi sasa haijapoteza mechi ikishuka dimbani mara 18, huku ikikusanya alama 48. Imewazidi mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Simba kwa alama 11 ambayo yenyewe imecheza mechi 17 na kukusanya alama 37. Aprili 30, mwaka huu, timu hizo zitapambana Uwanja wa Mkapa, Dar katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara. Kiungo wa zamani wa Simba raia wa Ghana, James Kotei, amezungumzia ubora wa Yanga ilionao msimu huu, huku akisema wanaweza kuwavua ubingwa Simba. “Kwanza nafurahi kuona ligi ya msimu huu ikiwa na ushindani mkubwa, binafsi nafurahi kuona Yanga ikitoa changamoto kubwa kwa Simba katika vita ya kuwania ubingwa, inaweza kufanikiwa. “Ushindani huu una faida kubwa sana kwenye kukuza thamani ya ligi, inawafanya wachezaji pia kupambana na ...

Mungu Tusaidie..Ajali Nyingine Mbaya Yaua WATU Sita Asubuhi ya leo

Image
Watu sita wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari (fuso) lenye namba T 239 AFB walilokua wakisafiria kuacha njia na kutumbukia kwenye korongo katika eneo la barabara ya Soni/Mombo wilayani Lushoto mkoani Tanga. Akizungumza na @ayotv_ kwa njia ya simu RPC wa Tanga, Safia Jongo amesema ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo March 29,2022. Aidha Kamanda Jongo amewataka Watumiaji wa vyombo vya Moto mkoani humo kuendelea kufuata sheria,kanuni na taratibu za usalama barabarani. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto na majeruhi wapo Hospitalini hapo wakiendelea kupata matibabu. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/DRld1Lv via IFTTT

Kauli Yamponza...Kamanda wa Polisi Aliyeomba Kuteuliwa na Rais Kuwa IGP Arudishwa Makao Makuu Kwa Uchuguzi

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro leo Machi 29, 2022 amefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa. Katika uhamisho huo, aliyekuwa RPC Mkoa wa Kagera, ACP Wankyo Nyigesa amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa RPC Rukwa, ACP William Mwampagale. Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, uhamisho huo umefanyika ili kupisha uchunguzi wa tukio la tarehe 26.3.2022 katika sherehe ya kumuaga ACP Wankyo ambapo alitoa maneno ambayo yanaonyesha kuwepo na ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozo ya Jeshi la Polisi. Pia katika mabadiliko hayo, Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Rukwa, ACP Theopista Mallya anakuwa RPC wa mkoani Rukwa aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Rukwa, ACP Mashenene Mayila anakuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa huo. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/MefoCkF via IFTTT

Wafunguka RPC aliyetamani cheo cha Sirro

Image
WADAU wametoa maoni yao juu ya kauli ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera (RPC) Wankyo Nyigesa, kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan kumteuwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania haliyakuwa (IGP) Simon Sirro bado anaihudumia nafasi hiyo. Baadhi walisema siyo jambo baya kwa mtu kutamani cheo fulani  huku wengine wakisema siyo sawa kutamani nafasi ya juu wakati aliyonayo hajaifanyia kazi ipasavyo. Mratibu wa Mtandao wa Kutetea Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumo, alisema mtu kutamani cheo cha juu siyo dhambi bali inaweza kutafsiriwa tofauti endapo atatumia njia za hujuma kupata nafasi anayoitamani. “Siyo vibaya kuomba kuteuliwa, huwenda kuna kitu kakiona kuwa hakiko sawa na kufikiri kuwa endapo atapatiwa nafasi hiyo anaweza kukirekebisha hivyo huo ni ujumbe kwa IGP aliyopo,” alisema Olengurumwa. Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga, alisema misingi ya kiutendaji kazi au cheo cha kuteuliwa hakiombi ila Rais humteua mtu pale a...

Wakenya Wenye Makasiriko "Mondi na Zuchu Wataachana tu"

Image
TETESI za penzi la mastaa wawili wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na msanii wake, Zuchu zimewafikia baadhi ya Wakenya wenye makasiriko ambao wametamka waziwazi; “Wataachana tu Hii ni baada ya gavana wa zamani wa Nairobi nchini humo, Mike Mbuvi Sonko ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii kuposti video ya Diamond au Mondi na Zuchu wakiimba wimbo wao maarufu wa Mtasubiri kwa kupokezana na kudekeana kimahaba. Katika video hiyo, Diamond na Zuchu wamekaa kwenye siti moja ya gari la kifahari aina ya Cadillac Escalade linalomilikiwa na jamaa huyo wakiimba Mtasubiri ambao ni miongoni mwa nyimbo kumi zinazopatikana kwenye albam fupi (EP) ya First Of All (FOA) ambayo Mondi ameachia hivi karibuni. Hata hivyo, baadhi ya wafuasi wa Sonko wameipokea video hiyo kwa hisia tofauti ambapo baadhi yao ambao waliamini Diamond atamrudia dada yao, Tanasha Donna ndiyo wamepatwa na makasiriko na kuanza kuwaombea wawili hao dua mbaya wakisema; “Wataachana tu!” Kwa miezi kadhaa sasa, Diamond na Zu...

Wanamuziki 8 Wanaoongoza Boomplay Kwa Idadi ya Wasikilizaji Wengi Africa, Tanzania Hatumo

Image
Kulingana na mtandao wa boomplay hii ni takwimu ya orodha ya wanamuziki 8' kutoka barani Africa wenye idadi kubwa ya streaming katika mtandao wa @boomplaymusic ambapo kwa kiasi kikubwa imetawaliwa na wanamuziki kutoka nchini nigeria. - 1. Burna Boy🇳🇬 - 217.3 million 2. Joeboy🇳🇬 - 216.5 million 3. Fireboy 🇳🇬- 198 million 4. Omah Lay 🇳🇬- 171.2 million 5. Olamide 🇳🇬- 162 million 6. Kizz Daniel 🇳🇬- 158.3 million 7. Davido🇳🇬 - 110.8 million 8. Wizkid 🇳🇬- 108.8 million Usisahau kuwa mwanamuziki @rayvanny ndie msanii pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki akiiwakilisha Tanzania 🇹🇿mwenye jumla ya streams million 100 katika mtandao huo wa boomplay. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Owyh5qD via IFTTT

Hatimaye #WillSmith Amemuomba Radhi Mchekeshaji ChrisRock Kwa Kumchapa

Image
Hatimaye #WillSmith Amemuomba Radhi Mchekeshaji #ChrisRock Kwa Kumchapa Kofi Siku Ya Jana Kwenye Tuzo Za Oscars Baada Ya Kuleta Utani Kuhusu Mke Wake. Kupitia Ukurasa wake Wa Instagram amekiri Ni Kweli Kuwa Alikosa Kufanya Kitendo Hicho na Kumuomba Jamaa Msamaha Hapo Awali Aliomba Radhi Kwa Oscars Wenyewe Pamoja Na Washiriki Wenzake Katika Tuzo Hizo 2022 Ameandika haya Kupitia Ukurasa Wake Instagram: "Violence in all of its forms is poisonous and destructive. My behavior at last night’s Academy Awards was unacceptable and inexcusable. Jokes at my expense are a part of the job, but a joke about Jada’s medical condition was too much for me to bear and I reacted emotionally. I would like to publicly apologize to you, Chris. I was out of line and I was wrong. I am embarrassed and my actions were not indicative of the man I want to be. There is no place for violence in a world of love and kindness.     I would also like to apologize to the Academy, the producers ...

Mpiga debe auawa kisa abiria

Image
Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia mpigadebe wa mabasi ya Abood Abdilah Yassin (32) mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kumuua mpiga debe mwenzake wakati wakigombea abiria kwenye stendi kuu ya mabasi Msamvu. Kamanda wa Polisi Mkoai Morogoro, Fortunatus Musilim amesema kuwa tukio hilo limetokea machi 28 majira ya saa 12 asubuhi katika stendi kuu ya mabasi Msamvu Manispaa ya Morogoro. Kamanda Musilim amemtaja aliyeuawa kuwa ni Tazani Mndeme (35) mkazi wa mwembesongo Manispaa ya Morogoro ambaye ni mpiga debe wa mabasi ya BM. Kamanda Musilim amesema walikuwa wakigombania abiria kwenye stendi hiyo na kwamba wapiga debe hao walianza ugomvi wa kugombea abiria na mtuhumiwa alimchoma kisu marehemu kifuani upande wa kushoto.   Amesema mara baada ya kuchomwa na kisu hicho watu waliokuwa kwenye tukio hilo walimkimbiza kwenye hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro ambapo alifariki wakati akindelea kupata matibabu. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/trdWZEv...

Chris Rock Akataa Kumfungulia Mashtaka Will Smith

Image
Mchekeshaji Chris Rock amekataa kufungua mashtaka dhidi ya Will Smith kwa kumpiga kofi jukwaani wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Oscar. Kwa mujibu wa ripoti, Idara ya Polisi jijini Los Angeles imesema ina taarifa za tukio hilo, na kwamba mhusika akibadili uamuzi, polisi watakamilisha ripoti ya uchunguzi. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/rhfacIb via IFTTT

Zijue Faida za Kunywa Maji Kabla ya Kula Chochote Unapoamka

Image
Kwanini ni muhimu kunywa maji? Miili yetu inaundwa na asilimia 70 ya maji, hivyo ni muhimu kunywa maji ya kutosha ili kuufanya mwili kufanya kazi vyema. Iwapo mwili wako haupati maji ya kutosha, hali hii inaweza kusababisha madhara mbalimbali ya muda mfupi na muda mrefu kama vile magonjwa ya shinikizo la damu, saratani pamoja na magonjwa ya figo. Ninawezaje kutumia maji kama tiba? Unaweza kutumia maji kama tiba ya matatizo mbalimbali kwa kufanya haya yafuatayo: Kunywa takriban Mililita 160 za maji kabla ya kuswaki au kula chochote mara tu unapoamka. Kunywa maji angalau dakika 30 kabla ya kula, lakini si ndani ya dakika 45 baada ya kifungua kinywa, chakula cha mchana au chakula cha jioni. Kama huwezi kunywa angalau bilauri 4 za maji basi anza na moja kisha ongeza taratibu kadri mwili wako unavyomudu. Karibu ufahamu faida 8 za msingi za kunywa maji kabla ya kula chochote unapoamka. 1. Huondoa sumu mwilini Unywaji wa maji mengi husaidia kuondoa sumu mwilini kwani huwe...

Will Smith Amchapa Kofi Chris Rock Jukwaani Kwenye Hafla ya Tuzo za Oscars

Image
Will Smith amchapa kofi Chris Rock jukwaani kwenye hafla ya tuzo za Oscars usiku wa kuamkia leo. Hii ni baada ya Chris Rock kuleta utani kwa mke wa Will Smith, Jada unaotajwa kumchefua Smith. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/UKJc6iS via IFTTT

Mkuu wa Jeshi: Urusi Haitafaulu Kuigawa Ukraine

Image
Mkuu wa idara ya ujasusi ya Ukraine ameonya kuwa Urusi ina njama za kutumia “mbinu za Korea” kwa Ukraine hii ni baada ya kushindwa kuuteka mji mkuu na kuiangusha serikali halali iliyo madarakani. Mkuu huyo wa idara ya ujasusi Jenerali Kyrylo Budanov anasema Urusi inanjama za kuigawanya Ukraine kama vile Korea ilivyogawanyika na kuzaa mataifa mawili ya Korea Kaskazini na Korea Kusini. Jenerali Budanov anasema baada ya mshambulizi ya Urusi kushindwa kupata matokeo waliotarajia sasa Rais Vladimir Putin analenga maeneo yalio mashariki pamoja na yale ya kusini mwa Ukraine . ‘Anasema ikiwa Putin atafaulu kuunganisha maeneo hayo mawili basi huenda akajaribu kuchora mpaka wa kuimega sehemu hiyo kutoka kwa Ukraine -kwa kiasi fulani ni kama vile ilivyotokea baada ya vita vya Korea.   Vita hivyo vilizaa Korea Kaskazini na Korea Kusini Lakini Jenerali Budanov anasema mpango huo wa Urusi kamwe hautafaulu. from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/1OgJhGA via IFTTT

Wachezaji 8 kutoka nje walivyoipamba Stars

Image
KWA mara ya kwanza kwenye historia ya soka Tanzania, Taifa Stars imekuwa na wachezaji wanane wanaocheza soka nje ya nchi. Wachezaji hao wameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa na wote walicheza kwenye mechi ya kirafiki iliyo kwenye Kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Jumatano iliyopita ilipoitandika Afrika ya Kati mabao 3-1, Uwanja wa Benjamin Mkapa. Baadhi walionekana kwa mara ya kwanza kuichezea Timu ya Taifa ya Tanzania, huku wengine wakiwa ni wale waliozoeleka. Wachezaji wote hao waliotoka nje walicheza, sita walianza, wawili wakiingia kipindi cha pili. Huenda kesho tena wakaonekana wakati timu hiyo itakapocheza tena mechi yake ya pili ya kirafiki ya kimataifa iliyo kwenye Kalenda ya FIFA dhidi ya Sudan. Huko nyuma, timu ya taifa ya Tanzania haijawahi kuita idadi kubwa kama hii ya wachezaji, wanaosakata kabumbu la kulipwa nje ya nchi kwenye michuano yoyote ile, iwe mechi za kirafiki, Kombe la Chalenji, kufuzu AFCON, au Kombe la Dunia.   Hawa ndiyo wac...

Download App ya Udaku Special Kuweza Kupata Habari za Udaku Kila Siku

Image
Usipitwe na Habari zetu za kila siku kwa kuzisoma kirahisi kupitia Application ya Udaku Special ambayo ipo Play Store kwa watumiaji wa Simu za Android Bonyeza Hapa Chini Kuinstall/Kudownload : ==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>> from UDAKU SPECIAL https://ift.tt/Ci7L5IM via IFTTT

Chid Benz ampa sifa Fid Q "Umeonyesha Busara, Heshima, Bila Kuwa Mbinafsi Wala Kukebehi mtu"

Image
  Rapa Chid Benz ameonyesha kufurahishwa na mwenendo wa rapa mwenzie Fareed Qubanda maarufu Fid Q  kufuatia namna alivyoweza kushughulikia na kutafuta suluhu ya sakata la uteuzi wa Steve Nyerere kama msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania. Chid Benz ameamua kuidhihirisha heshima yake kwa Fid Q kwa kitendo cha kuweza kuvumilia maneno makali na masimango kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo wadau pamoja wasanii wenzie. “Farid I like the fact umeweza control na kuonyesha yaliyo ndani yako busara, heshima, bila kuwa mbinafsi wala kukebehi mtu au watu huu ndiyo ukomavu uliyo ndani yako. Haijalishi mapungufu yaliyojitokeza (KAMA YAPO) umesimama kweli G. Hatukatahi kwenye game kuna sinto fahamu nyingi za kukatisha tamaa especially now na yanazidi kujitokeza siyo point yangu ya sasa,” alisema Chid. Chid Benz ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram kuchapisha ujumbe huo kama sehemu ya kuuthibitishia umma alichokiona kwa Fid Q katika kipindi chote cha changamoto hiyo. ...

Haji Manara "Wananchi Msiyumbishwe na Maneno ya Mitandaoni..Mwenzenu Nimejaliwa Moyo Mgumu wa Kustahmili Kashfa"

Image
  Msemaji wa Klabu ya Young Africans Haji Sunday Manara amewataka Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kupuuza mambo yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii na katika baadhi ya vyombo vya habari, yenye lengo la kuwatoa kwenye malengo yao Msimu huu 2021/22. Young Africans imeweka dhamira ya kutwaa Taji la Ligi Kuu Tanzania Bara Msimu huu, baada ya kulikosa kwa misimu minne mfululizo kwa kushuhudia likienda kwa Watani zao wa Jadi Simba SC. Manara amesema anaamini kuna makusudi inafanywa na baadhi ya watu ili kuikwamisha Young Africans isifikie lengo lake, hivyo amewasihi Mashabiki na Wanachama kuendelea kuwa kitu kimoja ili kufanikisha wanalolikusudia. “Wananchi wenzangu, interest yetu iwe kushinda Championship msimu huu, iwe kushinda FA na iwe kukamilisha Transformation yetu, mengine ni ya kupuuza.” “Nipo hapa kushirikiana na nyinyi kushinda Mataji, sipo hapa kujibizana na mtu, tuendelee kuwasamehe wanaotaka vurugu na malumbano coz bila kumtaja Haji kwa ubaya atamtaja na...

Okoa Ndoa Yako Sasa, Ongeza Nguvu za Kiume na Maumbile Kwa Njia Salama

Image
  Baadhi ya mambo yanayosababisha UPUNGUFU wa nguvu za kiume pamoja na maumbile madogo ya uume ni kama KISUKARI, KUJICHUA, NGIRI, KUTAZAMA VIDEO ZA NGONO, UNENE ULIOPITILIZA, ULAJI MBOVU N.K.     *DALILI NI KAMA:- 1.Kukosa ham ya tendo 2.Kuwahi kufika kelele ni 3.Kushindwa kurudia tendo 4.Uume kusinyaa katikati ya tendo 5.Kuchoka sana baada ya raundi moja 6.Uume kusimama kwa ulegevu     *TIBA ZILIZOTHIBITISWA:- 1.GING SENG PILLS @240,000/= >Hivi ni vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza ham na nguvu za kiume hata kwa wenye kisukari 2.TITAN GEL @240,000/= >Huongeza uume kwa 6-7 inch ndani ya wiki mbili 3.BIG PENIS, MAX MAN au GOOD MAN @270,000/= (Vidonge) >Huongeza uume, nguvu za kiume na kuimarisha misuli hata kwa waliothiriwa na kujichua 4.HANDSOME UP @270,000/= >Mashine hii huongeza uume kwa saizi unayotaka pamoja na kuimarisha misuli 5.VIGA SPRAY @180,000/= >Huchelewesha kufika kileleni na kuongeza parfomance. 6.S...