Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa mashabiki wamekuwa wakizishindanisha lebo za WCB Wasafi na Konde Music Worldwide kutokana na ushindani wa wamiliki wake katika Bongofleva. WCB Wasafi iliyomtoa Harmonize kimuziki mwaka 2015 ni ya Diamond Platnumz. Baadaye Harmonize alianzisha Konde Music na hapo ndipo ushindani ukaibuka. Hata hivyo, ukweli ni kwamba lebo hizi zina tofauti kubwa katika baadhi ya mambo kama ifuatavyo; 1. Hadi sasa WCB imefanikiwa kutoa albamu tatu na Extended Playlist (EP) nne za wasanii wake sita, huku Konde Music ikitoa albamu moja na EP tatu za wasanii wake wanne. 2. Konde Music imefanikiwa kumsaini msanii kutoka nje ya Tanzania, Young Skales (Nigeria) lakini WCB haijafanya hivyo, licha ya kuwapo taarifa za kufungua tawi lao Kenya. 3. Kwa sasa WCB inasimamia wasanii sita ambao ni Diamond, Rayvanny, Queen Darleen, Lava Lava, Mbosso na Zuchu, huku Konde Music ikisimama na wasanii sita ambao ni Harmonize, Ibraah, Young Skales, Cheed, Killy na Angella. ...