Haji Manara Atoa MPYA "Hivi Nikiondoka SIMBA Namuachia Nani Ukubwa wa Jina Langu Unaniponza?
Mkuu wa Idaya ya Habari na Mawasilino Simba SC, @hajismanara amewajibu baadhi ya wadau wa soka nchini ambao wamekua wakimtabiria mabaya kuhusu kazi zake ndani ya klabu hiyo. #Manara ametuma majibu hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kufuatia madai yaliyotolewa na baadhi ya wadau hao wakisema amesimamishwa kazi, huku akitakiwa kutozungumza lolote kuhusu Simba SC. #Manara ameeleza kuwa, bado yupo Simba SC, na ataendelea kufanya kazi zake kama kawaida, huku akiwatuliza mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. “Please Please Please (Tafadhali) Wanasimba mimi Haji wenu bado nipo nanyi na nitaendelea kuwa msemaji wenu hadi pale riziki yangu itakapokwisha, (Hatatokea mmoja wetu kubaki milele iwe kwa kifo au vinginevyo). “Waambieni wenye kuandika tetesi za kuondoka kwangu, mimi mtu dhaifu lakini ni mjuzi mno katika mambo ya mawasiliano ya umma na nina uzoefu mkubwa katika eneo hili na nishakuwa sugu na changamoto za kazi.” “Hala...